Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
3 2 8 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Katika hali ya kawaida, ili kupata faida kamili ya Mbinu ya Hatua Tatu ya ufasiri wa Biblia, lazima tujitoe kwamba tutajifunza kwa kina katika hatua moja: kuelewa muktadha wa asili . Kazi hii sio nyepesi wala rahisi kwa namna yoyote; maelfu ya miaka yanatutenganisha kutoka kwa waandishi na hadhira ya wakati wa kuandikwa andiko, na limeandikwa katika lugha ambazo ni ngeni kwetu na “zimekufa” Kwa namna ya kwamba haziendelei kuzungumzwa katika muundo ambao ziliandikwa. Asili ya lugha, utamaduni, na historia ni ngeni kabisa kwetu, na ukiongeza dhahania zetu wenyewe kuhusiana na ulimwengu wa kale, na kile tunachoita ukale na ukosefu wa mtazamo wa kisayansi wa ulimwengu, na tabia zetu zisizozuilika za kuusoma ulimwengu na masuala yetu kwa kuzingatia ya kwao yalivyokuwa. Inahitajika kuwa na kiasi kwa kiwango cha juu sana kuziweka sawa nadharia kuhusu ulimwengu wa Kale wa Biblia na kuufanyia utafiti kwa kuzingatia vigezo vyake wenyewe. Hiki ndicho kwa kifupi zana hizo zinaturuhusu kufanya; zinatoa fursa kwa mtafiti mnyeyekevu na aliyefungua ufahamu wake kuuona ulimwengu kutoka katika mtazamo wa wale waliokuwepo nyakati hizo, na kujaribu kuingia katika mawazo yao na kufikiri kama wao. Ubora tunaohitaji kukuza ndani yetu wenyewe na wanafunzi wetu ni ili kufaidika kikamilifu na nyenzo na zana za uhakiki wa kisasa ni kuvaa uhusika kana kwamba tupo kipindi hicho , sio sana kama wanazuoni walioziandika kazi hizo lakini ni kujihusisha na mazingira na watu mbao walikuwa wanawafanyia utafiti na kuandika kuwahusu. Kwa maneno mengine, lazima tuliendee andiko la Biblia na shauku ya kutaka kuelewa na kutengeneza maelewano na watu wa kipindi cha andiko. Ulimwengu wa kipindi andiko linaandikwa lazima uwe jambo letu la kwanza katika kujifunza, na kisha, baada ya kuwa tumejihusisha na na mazingira yao, tunaweza kuchota kanuni na kuhusianisha maana ya andiko na maisha yetu leo. Ili kuwasaidia wanafunzi waielewe kazi hii vizuri, utahitajika kuwa karibu na malengo ya somo, kwani zinaonyesha kwa undani namna ambavyo zana mbalimbali zinasaidia kutuunganisha na ulimwengu wa Kale pamoja na wakazi wake. Tunavyozidi kutaka kuingia kikamilifu na kwa usahihi katika ulimwengu wa nyakati za Biblia, ndivyo tutaweza kuzitendea kazi kanuni katika maisha yetu.
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker