Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

2 2 6 /

M U N G U B A B A

K I A M B A T I S H O C H A 3 3 Ufalme Wako Uje: “Hadithi ya Utukufu wa Mungu” Kuishi Chini ya Utawala Wake na Kufanya Umisheni Katika Ulimwengu Usio na Makanisa Mch. Dkt. Don L. Davis

I. Thamani ya Hadithi, Umuhimu wa Kisasili, na Ufalme wa Mungu

A. Wanadamu hufanya kazi kulingana na mifumo yao ya kutafsiri mambo: wanadamu wapo kama “mitazamo ya ulimwengu inayotembea.” 1. Kila kuwepo wa mwanadamu kimsingi ni “ulimwengu wenye mpangilio wa hadithi”. 2. Kutunga visasili kama tendo la mwanzo kabisa la wanadamu. 3. Jukumu la utamaduni: kutuwezesha kutunga uhalisia wetu kuanzia mwanzo. B. Kuunganisha taarifa: hadithi na hitaji la kuishi kwa kusudi. 1. Ufahamu wa kusudi: kuhusianisha vipengele vyote kwenye ujumla (kusudi kuu). 2. Ufahamu wa muda: kuhusiana na vipengele kama mambo ya jumla (makusudi makuu). C. Tatizo la falsafa ya upunguzaji katika Imani ( reductionism ) 1. Falsafa ya upunguzaji ( Reductionalism ) – kubadili maono ya kina ya imani ya Kikristo kuwa dhana, shughuli, mahusiano, au kipengele mbadala, kidogo, mara zote chenye mwelekeo wa kitamaduni. 2. Falsafa mantiki ( Rationalism ) – kutoa muda mwingi katika kutumia vithibitisho na hoja za kisayansi za kisasa ili kuipima imani katika Kristo, kupunguza imani ya Kikristo hadi kuwa sawa na kushikilia misimamo ya kimuktadha ya kimafundisho dhidi ya maoni mengine kinzani. 3. Dhana ya maadili ( Moralism ) – kupunguza maono ya Kikristo hadi kuwa tu adabu na maadili ya kibinafsi na ya kijumuiya, k.m., kuishi vyema katika muktadha wa familia ndogo (baba, mama, watoto), kushikilia msimamo fulani wa maoni fulani juu ya masuala kadhaa ya kimaadili yenye utata katika jamii.

Made with FlippingBook - Online catalogs