Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 2 3 1
M U N G U B A B A
Ufalme Wako Uje: “Hadithi ya Utukufu wa Mungu” (muendelezo)
6. Christus Victor : ufufuo wa Bwana mtukufu wa uzima, Mt. 28:1-15; Mk 16:1-11; Lk 24:1-12. F. Nyakati za Mwisho (kushuka kwa Roho Mtakatifu na zama zake) 1. Arabuni ya Mungu : Roho kama Ahadi na Ishara ya uwepo wa Ufalme, Efe. 1:13-14; 4:30; Mdo 2:1-47. 2. “Hili ni lile:” Petro, Pentekoste, na uwepo wa wakati ujao. a. Kanisa kama kionjo na wakala wa Ufalme wa Mungu, Flp. 2:14 16; 2 Kor. 5:20. b. Utawala wa sasa wa Masihi Yesu, 1 Kor. 15:24-28; Mdo 2:34; Efe. 1:20-23; Ebr. 1:13. c. Kuingizwa kwa jumuiya ya ufalme wa Mungu «katikati ya nyakati»; Rum.14:7. 3. Kanisa la Masihi Yesu: wageni katika Ufalme uliopo Tayari na ambao haujafika bado. a. Ukiri Mkuu: Yesu ni Bwana, Flp. 2:9-11. b. Agizo Kuu: nendeni mkafanye wanafunzi kati ya mataifa yote, Mt. 28:18-20; Mdo 1:8. c. Agizo Kuu: mpende Mungu na watu, Mt. 22:37-39. 4. Tangazo kuhusu Siri: Mataifa kama warithi wenza wa Ahadi, Rum. 16:25-27; Kol. 1:26-28; Efe. 3:3-11. a. Yesu kama Adamu wa Mwisho, kichwa cha jamii mpya ya wanadamu, 1 Kor. 15:45-49. b. Mungu akiwavuta kutoka ulimwenguni jamii mpya ya wanadamu, Efe. 2:12-22. 5. Katikati ya nyakati: ishara za Enzi ya Sabato na Yubile , Mdo. 2:17-., rej. Yoeli 2; Amosi 9; Eze. 36:25-27. G. Utimilifu wa Wakati (Ujio wa Pili wa Kristo), 1 Thes. 4:13-17. 1. Kukamilika kwa utume wa ulimwengu: uinjilishaji wa ethnoi za ulimwengu, Mt. 24:14; Marko 16:15-16; Rum.10:18.
Made with FlippingBook - Online catalogs