Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
2 3 2 /
M U N G U B A B A
Ufalme Wako Uje: “Hadithi ya Utukufu wa Mungu” (muendelezo)
2. Ukengeufu wa Kanisa, 1 Tim. 4:1-3;2 Tim. 4:3;2 Thes. 2:3-12. 3. Dhiki kuu, Mt. 24:21-; Lk 21:24. 4. Parousia : Ujio wa Pili wa Yesu, 1 Thes. 4:13-17; 1 Kor. 15:50-58; Lk 21:25-27; Dan. 7:13 5. Utawala wa Yesu Kristo duniani, Ufu. 20:1-4. 6. Kiti Kikuu cha Enzi Cheupe na Ziwa la Moto, Ufu. 20:11-15. 7. “Maana sharti amiliki yeye”: kuwekwa kwa mwisho kwa maadui wote chini ya miguu ya Kristo, 1 Kor.15:24-28. H. Baada ya Wakati (Milele Ijayo) 1. Uumbaji wa mbingu mpya na nchi mpya, Ufu. 21:1; Isa. 65:17-19; 66:22; 2 Pet. 3:13. 2. Kushuka kwa Yerusalemu mpya: makao ya Mungu yanakuja duniani, Ufu. 21:2-4. 3. Nyakati za kuburudisha: uhuru wenye utukufu wa watoto wa Mungu, Rum.8:18-23. 4. Bwana Yesu Kristo anaukabidhi Ufalme kwa Mungu Baba, 1 Kor. 15:24-28. 5. Enzi Ijayo: Mungu katika Utatu kama yote katika yote - Zek. 14:9; 2:10; Yer. 23:6; Mt. 1:23; Zab. 72:8-11; Mik. 4:1-3. A. Kusudi kuu la Mungu ni msingi wa historia yote ya wanadamu. 1. Lolote alipendalo, hulifanya, Zab.135:6. 2. Mashauri na mipango ya Mungu inasimama milele, kwa vizazi vyote, Zab. 33:11; Zab.115:3. 3. Mungu anatangaza mwisho wa vitu vyote tangu mwanzo, Isa. 46:10. 4. Hakuna kitu wala mtu awezaye kupinga mpango wa Mungu wa wokovu na ukombozi, Dan.4:35.
III. Matokeo ya Tamthilia ya Nyakati Zote
Made with FlippingBook - Online catalogs