Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 2 3 3
M U N G U B A B A
Ufalme Wako Uje: “Hadithi ya Utukufu wa Mungu” (muendelezo)
B. Mungu ndiye mhusika mkuu katika kufunuliwa kwa tamthilia ya kiungu, Efe.1:9-11. C. Umisheni ni urejesho wa kile kilichopotea mwanzoni mwa wakati . 1. Utawala mkuu wa Mungu, Mk 1:14-15. 2. Uasi wa Shetani, Mwa 3:15 pamoja na Kol. 2:15; 1 Yoh. 3:8. 3. Anguko la kuhuzunisha la wanadamu, Mwa.3:1-8 rej. Rum. 5:5-8. D. Kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi ni kutimiza jukumu letu katika muswada wa tamthilia ya Mwenyezi Mungu! A. Utofauti wa injili ya Yesu: “Ufalme umekaribia,” Mk 1:14-15. B. Yesu na kuanzishwa kwa Enzi Ijayo katika enzi hii ya sasa 1. Ujio wa Yohana Mbatizaji, Mt. 11:2-6. 2. Mwanzo wa huduma ya Yesu, Luka 4:16-21. 3. Makabiliano ya Yesu dhidi ya majeshi ya pepo, Luka 10:18-; 11:20. 4. Mafundisho ya Yesu na tamko lake la kuwa na mamlaka kamili duniani, Mk 2:1-12; Mt. 21:27; 28:18. C. “Ufalme umekuja na mtu mwenye nguvu amefungwa”: Mt.12:28, 29 1. Ufalme wa Mungu “umekuja” – pleroo 2. Maana ya kitenzi cha Kiyunani: “kutimiza, kukamilisha, kutimizwa, kama katika unabii” 3. Uvamizi, kuingia, udhihirisho wa uweza wa kifalme wa Mungu. 4. Yesu kama amfungaye mtu mwenye nguvu: Mt. 12:25-30 – Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, “Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama. 26 Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje? 27 Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu
Kifo cha Kristo kwa ajili ya dhambi zetu—malipo yake ya adhabu iliyotangazwa dhidi yetu—kilikuwa ushindi wake wa kisheria ambapo alifuta madai ya kisheria ya Shetani kwa wanadamu. Lakini Kristo pia alishinda ushindi wa nguvu. Yaani, Alipohesabiwa haki na kufanywa kuwa hai, na kutangazwa kuwa mwenye haki katika Mahakama Kuu ya ulimwengu, Shetani, adui mkuu wa Mungu na mwanadamu, alivuliwa silaha zote kabisa na kuondolewa utawala. Kristo aliibuka kwa ushindi kutoka katika gereza lile la zamani la wafu. Paulo anasema kwamba “akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.” (Kol. 2:15). ~ Paul Billheimer. Destined for the Throne . Minneapolis: Bethany House Publishers, 1996. uk. 87.
IV. “Ufalme wako Uje”: Kuishi Chini ya Utawala wa Mungu
Made with FlippingBook - Online catalogs