Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
2 3 4 /
M U N G U B A B A
Ufalme Wako Uje: “Hadithi ya Utukufu wa Mungu” (muendelezo)
hiyo hao ndio watakaowahukumu. 28 Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. 29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake. 30 Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya.” D. Aina mbili za udhiirisho wa Ufalme wa Mungu: Ufalme Uliopo/Ujao (Oscar Cullman, Christ and Time ; George Ladd, The Gospel of the Kingdom ) 1. Ujio wa kwanza : kufungwa kwa mwasi mkuu, kuporwa kwa nyumba yake, na kuja kwa utawala wa Mungu – yaani utawala wa Mungu uko hapa! 2. Ujio wa pili : kuharibiwa kwa yule mkuu mwasi, kuvurugika kwa utawala wake, na udhihirisho kamili wa uweza wa kifalme wa Mungu katika mbingu na dunia zilizoumbwa upya. V. Utaratibu wenye Msingi katika Kristo: Masihi Yeshua wa Nazareti kama Kitovu katika Ufunuo na Utawala wa Mungu. A. Kusudi la Masihi: Kuziharibu kazi za Ibilisi, 1 Yoh. 3:8. B. Kuzaliwa kwa Masihi: uvamizi wa Mungu dhidi ya utawala wa Shetani Lk 1:31-33. C. Ujumbe wa Masihi: Tangazo na kuzinduliwa rasmi kwa Ufalme, Mk 1:14-15. D. Fundisho la Masihi: maadili ya ufalme, Mt. 5-7. E. Miujiza ya Masihi: mamlaka na nguvu zake za kifalme, Mk 2:8-12. F. Utoaji pepo wa Masihi: kushindwa kwa Ibilisi na malaika zake Lk 11:14-20. G. Maisha na matendo ya Masihi: ukuu wa Ufalme Yoh. 1:14-18. H. Kukufuka kwa Masihi: ushindi na uthibitisho wa Mfalme, Rum. 1:1-4. I. Agizo la Masihi: wito wa kutangaza Ufalme wake ulimwenguni kote, Mt 28:18-20. J. Kupaa kwa Masihi: kutawazwa kwake, Ebr. 1:2-4.
Ujumbe wa Yesu ulikuwa Ufalme wa Mungu. Ulikuwa kitovu na muktadha wa yote aliyofundisha na kufanya.... Ufalme wa Mungu ndilo wazo kuu, mpango mkuu, kusudi kuu, nia kuu ambayo inakusanya kila kitu ndani yake na kukipa ukombozi, mshikamano, lengo, na kusudi. ~ E. Stanley Jones
Made with FlippingBook - Online catalogs