Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 2 3 5
M U N G U B A B A
Ufalme Wako Uje: “Hadithi ya Utukufu wa Mungu” (muendelezo)
K. Roho wa Masihi: arabuni (mdhamini, amana) ya Ufalme, 2 Kor. 1:20. L. Kanisa la Masihi: kionjo cha hali ijayo na wakala wa Ufalme, 2 Kor. 5:18-21 M. Wasaa wa Masihi mbinguni: uamiri wa jeshi la Mungu, 1 Kor. 15:24-28. N. Parousia ya Masihi (kurudi kwa pili): utimilifu wa mwisho wa Ufalme, Ufu. 19.
VI. Ufalme wa Mungu kama Uliopo na Unaotolewa Katikati ya Kanisa
A. Shekinah imetokea tena katikati yetu sisi kama hekalu lake, Efe. 2:19-22. B. Watu wa Mungu aliye hai ( ecclesia ) wanakusanyika hapa: watu wa Kristo mwenyewe kutoka katika kila ukoo, jamii, taifa, kabila, hali na utamaduni, 1 Pet. 2:8-9. C. Sabato ya Mungu inafurahiwa na kuadhimishwa hapa, uhuru, ukamilifu, na haki ya Mungu, Ebr. 4:3-10. D. Mwaka wa Yubile umefika: msamaha, kufanywa upya, na urejesho, Kol. 1:13; Mt. 6:33; Efe. 1:3; 2 Pet. 1:3-4. E. Roho ( arabuni ) anakaa ndani yetu: Mungu anaishi hapa na anatembea kati yetu hapa, 2 Kor. 1:20. F. Tunaonja nguvu za Enzi Ijayo: Shetani amefungwa katikati yetu, Laana imevunjwa hapa, ukombozi unapatikana katika Jina la Yesu, Gal. 3:10-14. G. Tunapitia shalom ya Ufalme wa milele wa Mungu: uhuru, ukamilifu, na haki ya utaratibu mpya vipo hapa, Rum. 5:1; Efe. 2:13-22. H. Tunatangaza habari njema ya utawala wa Mungu ( evanggelion ): tunawaalika wote wajiunge nasi tunaposafiri kuelekea udhihirisho kamili wa Wakati Ujao, Marko 1:14-15. I. Hapa tunapaza sauti “Maranantha!”: maisha yetu yameundwa na tumaini hai la wakati ujao wa Mungu na utimilifu, Ufu. 22:17-21.
Made with FlippingBook - Online catalogs