Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
2 3 6 /
M U N G U B A B A
Ufalme Wako Uje: “Hadithi ya Utukufu wa Mungu” (muendelezo)
VII. Ufalme Uliopo Tayari/Na Ujao (Angalia Mpangilio wa Theolojia ya Ufalme na Kanisa na Kuishi katika Ufalme Uliopo Tayari, Ambao Bado Haujaja kwenye viambatisho). A. Kupitia kufanyika mwili na Mateso ya Kristo, Shetani alifungwa. 1. Yesu amemshinda shetani 1 Yoh. 3:8. 2. Yesu amevishwa taji kama Bwana wa wote, Ebr.1:4; Fil. 2:5-11. 3. Shetani sasa amehukumiwa, Luka 10:17-21. 4. Nguvu za Shetani zimefanywa duni sana, Yak. 4:8. 5. Mamlaka yake imevunjwa, 1 Pet. 5:8. 6. Watumishi wake wanatawanywa, Kol. 2:15. 7. Mfumo wake unakatiliwa mbali, 1 Yoh. 2:15-17. 8. Wale aliowafanya watumwa wanawekwa huru, Kol. 1:13-14. 9. Hukumu yake ya mwisho imethibitishwa, Rum. 16:20. B. Ingawa Shetani ameshindwa, bado anaweza kusababisha madhara na anangojea siku ambayo ataharibiwa kabisa. 1. “Amefungwa, lakini kwa kamba ndefu,” 2 Kor. 10:3-5; Efe. 2:2. 2. “Kama simba angurumaye, lakini mgonjwa, mwenye njaa, na wazimu,” 1 Pet. 5:8. 3. Shetani anaendelea kuwa adui mwenye bidii wa Mungu na Ufalme. 4. Hupofusha fikira za wale wasioamini, 2 Kor. 4:4. 5. Hufanya kazi kwa njia ya udanganyifu, uwongo, na mashtaka Yoh. 8:44. 6. Anaingiza ushawishi wake katika mambo ya mataifa, 1 Yoh. 5:19 7. Anawakengeusha wanadamu wasifikie hatima zao walizokusudiwa, Mwanzo 3:1. 8. Huwakandamiza wanadamu kupitia manyanyaso, kashfa, woga, shutuma na kifo, Ebr. 2:14-15.
Kristo alipoketi mbinguni, alithibitisha kwa uhakika kwamba uharibifu wa Shetani ulikuwa umekamilika, na kwamba alikuwa amebatilishwa kabisa. hakunyang’anywa tu mamlaka na utawala wake wa kisheria, bali kwa nguvu kuu isiyo na kikomo alinyang’anywa silaha zake pia. Lakini haikuishia hapo tu. Yesu alipotoka katika gereza hilo lenye giza na “kupaa juu,” waamini wote waliinuliwa na kuketishwa pamoja naye. “Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu” (Waefeso 2:4-6). ~ Paul Billheimer. Destined for the Throne . Minneapolis: Bethany House Publishers, 1996. uk. 87. Kuzimu ilitupwa katika kufilisika kabisa. Shetani pamoja naye, akatuketisha
Made with FlippingBook - Online catalogs