Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 2 3 7
M U N G U B A B A
Ufalme Wako Uje: “Hadithi ya Utukufu wa Mungu” (muendelezo)
9. Huwapinga na kuwatesa watu wa Mungu, Efe. 6:10-18. C. Hukumu ya mwisho ya Shetani ni hakika na ya wakati ujao. 1. Ameharibiwa na kufedheheshwa kabisa kwa njia ya Msalaba, Kol. 2:15. 2. Kuondoshwa kwake kwa mwisho kutaletwa na Kristo wakati wa ule mwisho wa nyakati, Ufu. 20. 3. Umisheni ni tangazo na onyesho la kushindwa kwa Shetani kupitia Kristo. a. Huduma ya upatanisho, 2 Kor. 5:18-21. b. Huduma ya kufanya wanafunzi, Mt. 28:18-20. VIII. Wito wa Maisha ya Wokovu: Kuikumbatia Hadithi ya Mungu kama Hadithi Yako A. Wito wa Mungu kwa ajili ya wokovu na huduma unahusisha kushiriki kwa imani katika ahadi ya ufalme wa Mungu. 1. Wokovu kwa neema kwa njia ya imani, Efe. 2:8-10. 2. Toba: metanoia na uongofu, Mdo 2:38. 3. Kuzaliwa upya kwa Roho Mtakatifu wa Mungu, Yoh. 3:3-8; Tito 3:5. 4. Kuthibitisha hitaji letu la mfumo wa maisha wa kibiblia, kujifunza kwa nidhamu kuhusu Ufalme wa Mungu. Je, ninaishi uhuru, ukamilifu, na haki ya Ufalme ambayo ninawahubiria wengine? B. Wito wa Mungu kwa ajili ya wokovu na huduma unahusisha madhihirisho ya maisha ya Ufalme katika maisha binafsi na imani ya mtu. 1. Kama mtumishi mwaminifu na wakili wa siri za Mungu, 1 Kor. 4:1-2. 2. Kama Mkristo mcha Mungu katika tabia, maisha binafsi, na majukumu ya kifamilia, 1 Tim. 3; 1 Pet. 5:1-3; Tito 1. 3. Kama kaka au dada mpendwa katikati ya kusanyiko, 2 Kor. 8:22.
Made with FlippingBook - Online catalogs