Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

2 3 8 /

M U N G U B A B A

Ufalme Wako Uje: “Hadithi ya Utukufu wa Mungu” (muendelezo)

4. Kama ushuhuda wenye nguvu mbele ya wasioamini na walio nje, Kol. 4:5; Mt. 5:14-16. Je, katika maisha yangu ya binafsi na ya familia, katika mwenendo wangu katikati ya Mwili wa Kristo, kwa marafiki na jamaa zangu, na kwa majirani zangu mahali ninapoishi, ninaonyesha ushuhuda wa kuvutia wa maana ya kuwa mfuasi wa Kristo? C. Wito wa Mungu kwa aliji ya wokovu na huduma unahusisha kutengwa wakfu kwa maisha na mali za mtu ili kushuhudia na kuonyesha uhuru, ukamilifu, na haki ya Ufalme wa Mungu. 1. Utayari wa kuwa kila kitu kwa watu wote ili kuwaokoa baadhi, 1 Kor. 9:22-27. 2. Utayari wa kuteseka na hata kufa ili utawala wa Kristo utangazwe na kuenea, Mdo 20:24-32. 3. Kujitoa katika kuhakikisha unapatikana kwa Kristo bila masharti ili kutumika, kushuhudia kwa dhati neema na Injili kama Roho anavyoongoza (Yoh. 12:24; Mdo 1:8; Mt. 28:18-20). 4. Kusherehekea nia yenye neema ya Baba yetu na hatua ya kumshinda adui yetu, shetani. Je, nimejitoa bila masharti kwa Yesu Kristo ili nitumike kama mtumwa na chombo chake wakati wowote na popote anapoweza kuongoza ili ujumbe wa ufalme utangazwe na kuonyeshwa? D. Wito wa Mungu kwa ajili ya wokovu na huduma unahusisha maandalizi ya kuwa wakili wa siri za Mungu za Ufalme, Maandiko Matakatifu, na mafundisho ya Mitume. 1. Kutumia kwa usahihi Neno la kweli kama mtenda kazi wa Mungu, 2 Tim. 2:15. 2. Kusikia na kutii Maandiko matakatifu ambayo yanawakamilisha watakatifu kwa kila kazi njema, 2 Tim. 3:16. 3. Kutetea na kulinda ushuhuda wa kitume kuhusu Kristo na Ufalme wake, 2 Tim. 1:14 pamoja na Gal. 1:8-9 na 1 Kor. 15:1-4. Je, nimetumia wakati unaohitajika katika Neno na katika mafunzo ili kutayarishwa hata ninapowatayarisha wengine kwa ajili ya kazi ya huduma?

Made with FlippingBook - Online catalogs