Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

2 4 0 /

M U N G U B A B A

K I A M B A T I S H O C H A 3 4 Utatu wa Mungu katika Umoja: Utatu Mch. Dkt. Don L. Davis

“Kanisa halijasita kufundisha fundisho la Utatu. Bila kujifanya kwamba linaelewa, limetoa ushahidi wake, limerudia yale ambayo Maandiko Matakatifu yanafundisha. Baadhi wanapinga wakisema kwamba Maandiko hayafundishi Utatu wa Mungu kwa msingi kwamba wazo zima la Utatu katika umoja ni mkanganyiko wa maneno; lakini ikiwa hatuwezi kuelewa kuanguka kwa jani kando ya barabara au kuanguliwa kwa yai la ndege kwenye kiota kule, kwa nini Utatu uwe tatizo kwetu? ‘Tunamfikiria Mungu kwa kiwango cha juu zaidi’ anasema Michael de Molinos, ‘kwa kujua kwamba yeye hawezi kueleweka, na yuko juu ya ufahamu wetu, kuliko kumwelewa katika picha yoyote, au uzuri wa kiumbe chochote, kulingana na fahamu zetu potofu.’” Kanisa linaimba, “Utukufu kwa Baba, na kwa Mwana, na kwa Roho Mtakatifu.” Hii ni nini? Tunaomba na kutoa sifa kwa miungu watatu? Hapana; sifa kwa Mungu mmoja katika nafsi tatu. Kama vile wimbo unavyosema, “Yehova! Baba, Roho, Mwana! Uungu wa Ajabu! Utatu katika Umoja!” Huyu ndiye Mungu ambaye Wakristo humwabudu – Yehova wa Utatu. Kiini cha Imani ya Kikristo kwa Mungu ni ajabu iliyofunuliwa ya Utatu. Trinitas ni neno la Kilatini lenye maana ya utatu. Ukristo unasimama juu ya msingi wa fundisho la trinitas, sifa ya utatu, nafsi tatu za Mungu.” ~ J. I. Packer. Knowing God . Downers Grove: InterVarsity Press, 1993. uk. 65. Maswali ya Kutafakari • Kuna uhusiano gani kati ya kuelewa jambo na kutoa ushahidi kwa jambo fulani? • Unadhani ni kwanini ushuhuda bora zaidi wa Kanisa juu ya Utatu umebebwa katika nyimbo na ibada pamoja na kanuni na mafundisho yake? • Ni kwa jinsi gani uelewa mzuri wa asili ya siri na ajabu ni jambo la muhimu sana katika kujifunza fundisho la Utatu? • Kwa nini kumwelewa Mungu kama Utatu ni jambo la muhimu sana kwa ajili ya ukuaji wetu kiroho na vilevile ukuaji wa huduma zetu kwa wengine? ~ A. W. Tozer. The Knowledge of the Holy . New York: Harper Collins, 1961. uk. 18-19.

Made with FlippingBook - Online catalogs