Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

/ 2 4 1

M U N G U B A B A

Utatu wa Mungu katika Umoja: Utatu (muendelezo)

Baadhi ya Changamoto za Awali katika Kumtafakari Mungu kama Utatu • Siri hii ipo juu ya uwezo wetu kuelewa. • Haina kielelezo cha kidunia. • Usasa, baada ya usasa, na utawala wa sayansi: sifa ya zama zetu. • Kukosa ufahamu wa Biblia, kutokuwa na uzoefu wa kitheolojia, na kukosekana kwa mahubiri. Umuhimu wa Maajabu • Mungu haeleweki kabisa katika uhalisia wa alivyo. • Ni lazima tuvue viatu vyetu mbele ya nafsi kama hiyo. • Mwisho wa tafakari ya namna hiyo si mahesabu bali ni ibada. Haja ya Unyenyekevu • Maandiko, ambayo ni kanuni yetu ya imani na utendaji, hayana makosa. • Mafundisho ya kanisa lazima yatuongoze kweli. • Hatimaye, lazima nia zetu, na si akili zetu, zishinde hali yetu ya kutokuwa na uwezo kibinadamu kuelewa yale ambayo hayawezi kueleweka kikamilifu. Fundisho la Utatu ni ukweli kwa ajili ya moyo. Ni roho ya mwanadamu pekee inayoweza kuingia kupitia pazia na kupenya ndani ya Patakatifu pa Patakatifu. “Acha nikutafute kwa kutamani” Anselm alisihi, “nikutamani katika kukutafuta; acha nikupate katika upendo, na kukupenda katika kukupata.” Upendo na imani vimetulia katika fumbo la ajabu za Uungu. Wacha ufahamu wa kawaida upige magoti kwa heshima hadharani. ~ A. W. Tozer. The Knowledge of the Holy . uk. 20.

Made with FlippingBook - Online catalogs