Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

/ 2 4 3

M U N G U B A B A

Utatu wa Mungu katika Umoja: Utatu (muendelezo)

B. Uungu wa Watatu unathibitishwa (Erickson, uk. 98). Kila nafsi ya Mungu, (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu) inaelezwa kuwa na sifa ambazo zinathibitishwa kuwa ni za Mungu pekee. 1. Baba ni Mungu (imethibitishwa kote ulimwenguni). 2. Mwana ni Mungu (Flp. 2:5-11; Yoh. 1:1-18; Ebr. 1:1-12; Yoh. 8:58, nk.). 3. Roho Mtakatifu ni Mungu (Mdo 5:3-4; Yoh. 16:8-11; 1 Kor. 12:4-11; 3:16-17; Mt. 28:19; 2 Kor. 13:14). 4. Nafsi zote hizi tatu za utatu wa kibiblia zina sifa zinazofanana. a. Umilele, Rum. 16:26 pamoja na Ufu. 22:13; Ebr. 9:14. b. Utakatifu, Ufu. 4:8, 15:4; Mdo 3:14; 1 Yoh. 9:14. c. Kweli, Yoh. 7:28; Yoh. 17:3; Ufu. 3:7. d. Kuwepo kila mahali, Yer. 23:24; Efe. 1:23; Zab. 139:7. e. Kuweza yote, Mwa. 17:1 pamoja na Ufu. 1:8; Rum. 15:19; Yer. 32:17. f. Kujua yote, Mdo 15:18; Yoh. 21:17; 1 Kor. 2:10-11. g. Uumbaji, Mwa. 1:1 pamoja na Kol. 1:16; Ayu. 33:4; Zab. 148:5 pamoja na Yoh. 1:3, na Ayu. 26:13. h. Chanzo cha uzima wa milele Rum. 6:23; Yoh. 10:28; Gal. 6:8. i. Kumfufua Kristo kutoka kwa wafu, 1 Kor. 6:14 pamoja na Yoh. 2:19 na 1 Pet. 3:18. C. Mungu kama WATATU?: makisio ya kimantiki au mafundisho ya kibiblia (Erickson, uk. 99) 1. Vidokezo vya maandiko: changamoto ya 1 Yohana 5:7. 2. Muundo wa wingi wa jina la Mungu: Elohim, Mwa. 1:26, Isa. 6:8. 3. Imago Dei katika mwanadamu, Mwa. 1:27 pamoja na 2:24. 4. Kutaja majina sawa: umoja na wingi, Mt. 3:16-17; 28:19; 2 Kor. 13:14.

Made with FlippingBook - Online catalogs