Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

/ 2 4 5

M U N G U B A B A

Utatu wa Mungu katika Umoja: Utatu (muendelezo)

4. Kabla ya ubatizo wake, Yesu alikuwa mtu wa kawaida tu (ingawaje muadilifu) rej. Mt. 3:16-17. 5. Wakati wa ubatizo, Roho alishuka juu ya Yesu na nguvu za Mungu zilitiririka kupitia yeye 6. Mtazamo huu haujawahi kuwa maarufu. C. Modalistic Monarchianism 1. Kuna Mungu mmoja ambaye anaweza kutajwa kama Baba, au Mwana, au Roho. 2. Majina haya hayasimami kwa ajili ya utofauti halisi wa nafsi au washiriki tofauti, bali ni majina ya Mungu kila moja likifanya kazi kwa nyakati tofauti. 3. Baba, Mwana, na Roho ni ufunuo endelevu, unaofanana wa nafsi moja. 4. Nafsi moja yenye majina, shughuli, au wajibu tofauti. 5. Mtazamo huu hautoshi kuchukua taarifa kamili za kibiblia kwa umakini. D. Maelezo Sahihi (Erickson, uk. 102-103) 1. Mtaguso wa Constantinople (381) na maoni ya Athanasius (293 373) na “mababa wa Kapadokia” (Basil, Gregory wa Nazianzus, na Gregory na Nyssa). 2. Ousia [kiini] moja katika hypostases [nafsi] tatu (kiini kimoja, lakini nafsi tofauti zaidi ya moja). a. Mungu yupo katika asili moja pekee. b. Mungu yuko kwa wakati mmoja na huohuo katika namna au uhalisia au hypostases (nafsi) tatu. 3. Mkazo wa Kapadokia a. Hypostases (nafsi) moja moja ndiyo ousia (kiini) ya Uungu. b. Kila nafsi hutofautishwa kutokana na tabia au sifa ambazo ni za kipekee kwake (kama mtu binafsi alivyo ukilinganisha na watu wote).

Made with FlippingBook - Online catalogs