Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

2 4 6 /

M U N G U B A B A

Utatu wa Mungu katika Umoja: Utatu (muendelezo)

4. Sio tri-theism : imani kwa miungu watatu. Kwa nini? a. “Kama tunaweza kupata shughuli moja ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ambayo kwa namna yoyote haina tofauti katika nafsi yoyote kati ya hizo tatu, lazima tuhitimishe kwamba kuna (kiini) asili moja tu inayofanana ambayo inahusika” (Erickson, uk. 102). b. Nafsi za Utatu zinaweza kutofautishwa kiidadi kama nafsi, lakini haziwezi kutofautishwa katika asili au kiini chao (wako tofauti katika nafsi, ila ni mmoja katika asili).

III. Vipengele Muhimu, Mifano, na Matokeo ya Utatu (Erickson, 103)

A. Vipengele Muhimu

1. Mungu ni mmoja, sio kadhaa. 2. Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu kila mmoja ni wa Kiungu. (Kila mmoja ana sifa na tabia za Mungu mmoja wa kweli. 3. Umoja wa Mungu na utatu wa Mungu, kwa kweli, havipingani). 4. Utatu ni wa milele. 5. Utii baina ya nafsi za Utatu hautoi maana ya udogo au wa hadhi ya chini katika asili yao. a. Mwana yuko chini ya Baba b. Roho yuko chini ya Baba c. Roho yuko chini ya Mwana kama alivyo chini ya Baba d. Nafasi hizi ni kwa ajili ya utendaji tu; kule kuwa chini ya mwingine hakuzungumzi juu ya udogo. 6. Utatu haueleweki.

Made with FlippingBook - Online catalogs