Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
2 4 8 /
M U N G U B A B A
K I A M B A T I S H O C H A 3 5 Ukuu wa Mungu na Ufunuo kwa Ulimwengu Nadharia Kinzani Kuhusu Mungu na Ulimwengu Mch. Dkt. Don L. Davis
Sijaribu, Bwana, kupenya katika utukufu wako, kwa maana ufahamu wangu haufikii hilo. Lakini ninatamani kwa kiasi fulani kuelewa kweli yako, ambayo moyo wangu unaamini na kuipenda. Kwa maana sitaki kufahamu ili nipate kuamini, bali naamini ili nipate kuelewa. Kwa maana hili nalo naamini, ya kwamba nisipoamini, sitaelewa. ~ Anselm. Proslogion 1 . Anselm wa Canterbury, Toleo la 1: Monologion, Proslogion, Debate with Gaunilo, and a Meditation on Human Redemption . Imehaririwa na Kutafsiriwa na Jasper Hopkins na Herbert W. Richardson. New York: The Edwin Mellen Press, 1975. uk. 93. Mpangilio sahihi ni kuamini mambo mazito ya imani ya Kikristo kabla ya kuanza kuyajadili kwa ufahamu wa kawaida. Lakini tunaghafilika ikiwa, tukiwa tumeufikia uthabiti wa imani, hatutafuti kuelewa kile tunachoamini. Kwa neema ya Mungu iliyotangulia na kuniandaa kwa ajili ya wokovu, ninajiona kushikilia imani ya ukombozi wetu, ili hata kama ningeshindwa kabisa kuuelewa, kusiwe na kitu kinachoweza kutikisa uthabiti wa imani yangu. Tafadhali nionyeshe ni nini, kama unavyojua, wengine wengi wote pia wanatafuta kujua: Kwa nini Mungu, ambaye ni muweza wa yote, achukue udogo na udhaifu wa asili ya mwanadamu ili kuifanya upya? ~ Anselm. Cur Deus Homo (Boso kwa Anselm) 1:2. Why God Became Man and The Virgin Conception and Original Sin , cha Anselm wa Canterbury. Albany, NY: Magi Books, 1969. uk. 65. Maswali ya Kutafakari • Kulingana na Anselm, kuna uhusiano gani kati ya kuamini na kuelewa ukweli wa imani ya Kikristo? • Kwa nini Anselm anaamini kuwa ni makosa kutohusisha ukweli wa imani yetu ya Kikristo katika viwango vya kina vya mantiki na hoja? • Je, ni nini muhimu zaidi kwa uelewa wa kitheolojia: kutafakari kwetu ukweli tunaouelewa au kujitoa kwetu kuelewa ukweli tusioufahamu? Eleza jibu lako.
Made with FlippingBook - Online catalogs