Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 2 5 1
M U N G U B A B A
Ukuu wa Mungu na Ufunuo kwa Ulimwengu (muendelezo)
C. Changamoto za Theolojia ya Asili 1. Uthibitisho unaweza kufanya kazi dhidi yetu : una uvujaji na nyufa (Erickson, uk. 37). 2. Mawazo yaliyomo yanaweza kuwa yasiyoweza kuthibitishwa (Erickson, uk. 37). 3. Baadhi yana kasoro za kimantiki : unaweza kutetea hoja kwa ufanisi kwa kutumia kinachoonekana kuthibitisha kile ambacho hakiwezi (au hakijapata) kushuhudiwa? (Erickson, uk. 37) 4. Maelezo mengine mbadala yanashughulika na ushahidi huo huo kwa njia tofauti: teleolojia dhidi ya mabadiliko (Erickson, uk. 38). 5. Je, uthibitisho unaonyesha huyo Mungu ni Mungu wa aina gani? (Vipi kuhusu kuwepo kwa uovu, “ theodicy ”?) (Erickson, uk. 38) D. John Calvin: Ufunuo wa Jumla bila Theolojia ya Asili (Erickson, uk. 39) 1. Ufunuo wa Mungu kwa asili unajitegemea na ni halali . 2. Kwa sababu ya dhambi na mapungufu ya mwanadamu yatokanayo na dhambi hiyo, wanadamu hawawezi kumjua Mungu vya kutosha katika ufunuo huo wa jumla (Erickson, uk. 39). 3. Hali ya ukosefu wa kibinadamu , kwa hivyo, huzuia ufanisi (yaani, mafanikio, utoshelevu) wa ufunuo wa jumla kwa wanadamu ambao hawajazaliwa upya (Erickson, uk. 40). 4. Tunahitaji “ miwani ya imani ” (Erickson, uk. 40). E. Je, ufunuo wa jumla unaweza kutoa maudhui ya kutosha kwa mtu kuokolewa? 1. Hoja zinazopinga a. Vipi kuhusu imani binafsi katika Yesu Kristo? b. Vipi kuhusu umuhimu wa Warumi 10? c. Vipi kuhusu msukumo wa kwenda “ulimwenguni kote?” (Rej. Mt 28:18-20).
Kimsingi, haya ni maoni kwamba Mungu ametupa
ufunuo huru, halali, wa kiufahamu juu yake mwenyewe katika uumbaji asilia, historia, na haiba ya kibinadamu. Upo kwa yeyote anayetaka kuuangalia. Ufunuo wa jumla si kitu kinachosomwa katika asili na wale wanaomjua Mungu kwa misingi mingine;
tayari upo kupitia uumbaji na upaji
endelevu wa Mungu. ~ Erickson, uk.39.
Made with FlippingBook - Online catalogs