Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 2 5 3
M U N G U B A B A
Ukuu wa Mungu na Ufunuo kwa Ulimwengu (muendelezo)
E. Kweli ya kibiblia na uumbaji vyote ni ufunuo wa Mungu, na vinahusiana na kukamilishana (Erickson, uk. 42). 1. Mungu ndiye chanzo cha aina zote za ufunuo. 2. Kama vyanzo vya ukweli kumhusu Mungu, vinakamilishana na kujalizana. F. Ujuzi na maadili ya kibinadamu, kwa kiwango ambacho ni vya kweli na sahihi, vyote hutoka kwa Mungu (Erickson, uk. 42). 1. Ukweli wote kila mahali katika kila eneo ni ukweli wa Mungu. 2. Kila kilicho sahihi katika kila nyanja huakisi haki yaMungumwenyewe. 3. Ujuzi wa kibinadamu na kilicho sawa kimaadili ni “cheche” kutoka katika mwako wa Mwenyezi.
Made with FlippingBook - Online catalogs