Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 5 5
M U N G U B A B A
Hitimisho
1 Tim. 1:17 Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina
» Mungu Baba Mwenyezi ndiye mwenye mamlaka kuu na utawala juu ya uumbaji wote na historia. » “Uangalizi na utunzaji” wa Mungu unarejelea ukweli kwamba Mungu ndiye atendaye mapenzi yake makuu katika ulimwengu ambapo matukio yote yamepangwa naye kutimiliza kusudi lake jema kwa ajili yake na uumbaji. » Baba Mwenyezi ndiye Bwana mwenye enzi juu ya yote, chanzo cha uhai wote, na Mtegemezaji mwenye uweza wote kupitia Mwanawe, Yesu Kristo. Tafadhali chukua muda wa kutosha kujibu maswali haya na mengine yaliyoibuliwa kupitia video. Sehemu hii inasisitiza hasa “Uungu” wa Mungu, yaani, wazo la kwamba Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu ndiye Bwana Mtawala wa vitu vyote, anayeumba, anayetegemeza, na kutoa mahitaji kwa vitu vyote vilivyo katika uumbaji. Kweli ya hali ya juu namna hiyo itachochea shauku, au kuibua maswali yanayohitaji ufafanuzi. Kama kawaida, kuwa wazi na toa majibu yako kwa ufupi, na inapobidi, tumia Maandiko kuunga mkono. 1. Ni kwa namna gani umiliki wa Mungu kwa dunia na ulimwengu kama Muumba huturahisishia kumwelewa kama mwenye mamlaka juu ya vitu vyote? 2. Ikiwa uumbaji ni mali ya Mungu, na ikiwa aliumba mbingu na nchi, ni kwa nini basi kila kitu hakifanyiki kama Mungu atakavyo nyakati zote? 3. Inamaanisha nini tunaposema kwamba Mungu hutenda kazi katika uumbaji kwa ajili ya makusudi yake mwenyewe? Je, hii inamaanisha kwamba Mungu analo kusudi katika matetemeko ya ardhi, na vimbunga vikubwa vinavyoua mamia ya watu kila mwaka? 4. Pamoja na vita zote na uharibifu katika historia ya mwanadamu, tunawezaje kusema kwamba Mungu hufanya kila kitu duniani kulingana na mapenzi yake mwenyewe? 5. Neno “uangalizi na utunzaji” linamaanisha nini? Ni kwa namna gani dhana hii inaweka wazi uhusiano wa Mungu na ulimwengu wake aliouumba?
2
Sehemu ya 1
Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu
Made with FlippingBook - Online catalogs