Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

5 6 /

M U N G U B A B A

6. Kulingana na Maandiko, kwa nini Mungu anao uwezo wa kuwa chanzo na mpaji wa vitu vyote? Mungu anawezaje kutegemeza vitu vyote na bado asipoteze nguvu yoyote au kuonyesha udhaifu katika nafsi yake? 7. Bwana wetu Yesu anao wajibu gani katika kazi endelevu ya Mungu kutegemeza vitu vyote? Yesu alikuwa na wajibu gani katika uumbaji wa ulimwengu wote? 8. Ni lipi kusudi moja na lisilopingika la vitu vyote katika uumbaji? Tunajuaje kwamba ulimwengu kwa hakika utatimiza kusudi hili kuu?

Mungu kama Muumba: Uangalizi na Utunzaji wa Mungu Sehemu ya 2: Umuhimu wa Ukiri wa Nikea

2

Mch. Dkt. Don L. Davis

Mungu hudhihirisha uangalizi na utuzanji wake mkuu kupitia uhifadhi na usimamizi wake kwa vitu vyote. Kusema kwamba Mungu huhifadhi vitu vyote kunamaanisha kuwa vitu vyote vipo na vinashikamana pamoja kwa nguvu kuu ya utunzaji na uangalizi wa Mungu. Vivyo hivyo, tunaposema kwamba Mungu huvisimamia vitu vyote tunathibitisha kwamba Mungu anayo mamlaka na huyatumia katika ulimwengu wote, akifanya chochote anachokusudia katika uumbaji wake. Lengo letu katika Sehemu hii, Umuhimu wa Ukiri wa Nikea, ni kukusaidia uone kwamba: • Kazi maalum ya uangalizi na utunzaji wa Mungu inafunuliwa katika uhifadhi na usimamizi wake wa vitu vyote. • “Uhifadhi” unarejelea ukweli kwamba vitu vyote kwa hakika vipo na vinashikamana pamoja kwa nguvu kuu ya utunzaji na uangalizi wa Mungu. • Bila kujali nadharia zinazotolewa kuhusu chimbuko la ulimwengu, hakuna mtu na hakuna kitu kinachoweza kudai kwa namna yoyote kuwa na uwezo wa kujitegemea mbali na Mungu aliye chanzo cha viumbe vyote. • “Utawala” unarejelea ukweli kwamba Mungu nidye mwenye enzi juu ya ulimwengu mzima, akiwa na mamlaka yote kufanya chochote anachokusudia katika uumbaji.

Muhtasari wa Sehemu ya 2

Made with FlippingBook - Online catalogs