Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 5 7
M U N G U B A B A
• Mungu ataurejesha uumbaji wake kutoka katika hatari ya uovu wakati wa kurudi kwenye utukufu kwa Kristo. • Mafundisho sahihi kuhusu uangalizi na utunzaji wa Mungu hutatua baadhi ya makosa ya kisasa ya falsafa na theolojia, mfano, imani kwamba Mungu ni sawa na uumbaji wake ( pantheism ), imani kwamba Mungu aliyeumba ulimwengu hajihusishi tena na mambo ya ulimwengu ( deism ), mtazamo kwamba matukio yote ya zamani, ya sasa na ya baadaye, yamepangwa tayari na Mungu na kwa sababu hiyo hayawezi kuepukika ( fatalism ), na msimamo kwamba mambo yote hutokea kwa bahati nasibu ( chance ).
I. Kazi Maalum ya Uangalizi na Utunzaji wa Mungu Inafunuliwa katika Uhifadhi wake wa vitu Vyote.
Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video
2
A. Ufafanuzi wa uhifadhi wa Mungu wa vitu vyote ulimwenguni
Kanuni ya Imani ya Nikea kuhusu nafsi ya Mungu Baba: “Tuna mwamini Mungu mmoja, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.”
1. Uhifadhi = vitu vyote vipo na vinashikamana pamoja kwa nguvu kuu ya utunzaji na uangalizi wa Mungu. Hakuna kitu kingeweza kuendelea kuwepo bila upaji na utegemezaji binafsi wa Mungu kwa ajili ya uzima.
2. Hakuna kitu na hakuna mtu mwenye uzima ndani yake ambao ni kwake mwenyewe, Zab. 104:27-32.
3. Vitu vyote hufanya kazi kwa msingi wa mapenzi ya Mungu yaliyoruhusiwa pekee.
a. Hakipo ambacho kingedumu pasipo utunzaji endelevu wa Mungu, Ayubu 34:14-15.
b. Uzima wa mwanadamu haujitegemei, Zab. 146:4.
c. Mauti inapovipata viumbe vilivyo juu ya nchi, miili yao hurejea mavumbini, na uhai wao humrudia Mungu, Mhu. 12:7.
Made with FlippingBook - Online catalogs