Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

1 4 4 /

THEOLOJIA YA KANISA

³ Kupitia taswira ya Kanisa kama familia na nyumba ya Mungu, tunaona kwamba tunapaswa kuishi kama kaka na dada kwa umoja kama familia pendwa ya Mungu mwenyewe. ³ Kama mwili wa Kristo ulimwenguni, sisi Kanisa tunapaswa kudhihirisha maisha ya Yesu katika mahusiano yetu kati ya washirika wetu, na kwa namna tunavyoishi na majirani zetu. ³ Kanisa ni hekalu la Roho Mtakatifu, watu watakatifu walioitwa kufuata matendo ya utakatifu na utii kama mahali patakatifu ambapo Jina la Mungu linajulikana na kutukuzwa. ³ Kama mabalozi wa Kristo, Kanisa limeitwa kuwakilisha mamlaka na utawala wa Mungu ulimwenguni. Tumeitwa kuonyesha utawala wa uadilifu wa Ufalme huo kupitia kazi zetu za uhuru, uzima (ukamilifu), na haki. ³ Kanisa linafafanuliwa kama jeshi la Mungu, jambo ambalo linaangazia jukumu lake la kupigana kama askari wa Mungu katika vita vya Mwana Kondoo, kwa kutangaza kweli ya Mungu katika Kristo, kwa kufanya kazi kwa njia ya Neno kuharibu kazi ya ibilisi, na kwa kushinda uovu kwa wema. Sasa ni wakati wa wewe kujadili na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu ufahamu wako wa utambulisho na kazi ya Kanisa. Mtazamo wako juu ya jukumu na uwezo wa Kanisa una athari kubwa juu ya maisha na huduma yako. Ni muhimu kwamba uthamini kikamilifu kweli hizi zilizojaa utajiri zinazohusiana na Kanisa. Kama viongozi, kazi yetu ni kuwasaidia wengine katika Kanisa kugundua karama na wajibu wao katika mwili, ili tuweze kukua katika mambo yote katika Kristo huku kila mmoja akifanya kazi katika nafasi yake ipasavyo. Ni vigumu kuwasaidia wengine kuelewa umuhimu wa Kanisa ikiwa wewe mwenyewe una mtazamo wa chini au usio sahihi kuhusu utambulisho wa Kanisa na kazi yake duniani. Andaa orodha yako mwenyewe ya maswali mahususi ambayo yanaweza kukusaidia kupata ufahamu bora na kamili wa jukumu la Kanisa ulimwenguni. Je, una maswali gani hasa kwa kuzingatia mambo ambayo umejifunza hivi punde? Labda baadhi ya maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi. * Je, ni kwa kiwango gani tunapaswa kujihusisha na kuzingatia vigezo hivi vya “ziada vya nje ya Biblia” kuhusu Kanisa (yaani, vigezo vya Kanuni ya Imani ya Nikea, Matengenezo ya Kanisa na Kanuni ya Vicent)? Je, tunapaswa kuelewa na kuthamini vipi uhusiano wa vigezo hivi na kile

4

Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Wanafunzi

ukurasa 265  13

Made with FlippingBook - Share PDF online