Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
2 2 4 /
THEOLOJIA YA KANISA
Uhusiano huu mpya wa kuwa “ndani ya Kristo” ulitangazwa kwa mara ya kwanza na Bwana kwa wanafunzi wake katika chumba cha juu katika kauli, “Ninyi ndani yangu [en emoi], nami ndani yenu” (Yohana 14:20). Uhusiano mpya wa mwamini katika Kristo unafafanuliwa kama nafasi mpya, “katika Kristo,” inayotokana na kazi ya Mungu. Ufunuo wa ushirika wa karibu kupitia maneno “Mimi ndani yenu” unadhihirisha kwamba hii ni zaidi ya nafasi tu iliyoanzishwa kwa mapenzi ya kimungu. Hilo limezaa fundisho la “muungano” au “kuungamanishwa” na Kristo, neno ambalo kwa kawaida huchukuliwa kama kisawe cha utambulisho. Mifano mbalimbali imetumika katika Maandiko ili kuonyesha muungano na utambulisho huu. Mzabibu na matawi vimetumiwa na Kristo mwenyewe katika Yohana 15:1-6.... Kielelezo kingine ni kile cha kichwa na mwili (rej. Efe. 1:22-23; 4:12-16; 5:23-30.... Semi mbalimbali zimetumiwa kuashiria utambulisho huu. Iliyo tumika mara nyingi zaidi ni istilahi “katika Kristo” (en Christo), lakini nyingine pia zimetumika kama vile “katika” au “ndani ya Kristo” (eis Christon) na “katika Bwana”(en kyrio).” ~ J. F. Walvoord. “Identification with Christ.” Evangelical Dictionary of Theology . Grand Rapids: Baker, 1984. uk. 542
12 Ukurasa 28 Kipengele namba III-A
1 Yohana 3:24a - Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. (Taz. Efe. 1:1-14 na Kol. 2:6-10 kwa vifungu vinavyoendeleza zaidi dhana ya “ndani yake”).
13 Ukurasa 29 Kipengele namba III-B
Kumbuka kwamba ifuatayo ni tafsiri ya Maandiko kwa njia ya mifano ( typological interpretation ). Tafsiri ya Kitaipolojia ya Biblia inatokana na utambuzi kwamba matukio, watu, na maeneo ambayo yanaonekana mapema katika historia ya wokovu yanafanyika mifano ambayo kupitia hiyo matukio ya baadaye yanafasiriwa. Tukio la Kutoka (ambalo linahusisha Pasaka, kuvuka Bahari ya Shamu, na safari ya jangwani kwenda Kanaani) lina historia ndefu ya kutumika kama kielelezo katika tafsiri ya Kikristo ya Maandiko. Matumizi haya yanarejea kwa Paulo mwenyewe aliyeandika: 1 Kor. 10:1-4 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; 2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; 3 wote
14 Ukurasa 33 Kipengele namba IV-D
Made with FlippingBook - Share PDF online