Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 2 2 5

THEOLOJIA YA KANISA

wakala chakula kile kile cha roho; 4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.

Zilizoorodheshwa katika sehemu hii ni kweli za msingi zilizoandikwa kwa namna ya sentensi ambazo wanafunzi wanapaswa kupokea kutokana na somo hili, yaani, kutokana na video na mazungumzo ambayo umeyafanya pamoja nao chini ya mwongozo wako. Hakikisha kwamba dhana hizi zimefafanuliwa kwa uwazi na kuzingatiwa kwa uangalifu, kwani maswali ya majaribio na mitihani yataundwa moja kwa moja kutokana na maudhui haya. Kilicho muhimu zaidi ni kuwasaidia wanafunzi kupata uzoefu wa kina wa mawazo haya ili waweze kuyafahamu zaidi na zaidi. Uzoefu huu utakuwa muhimu kwao wanapoendelea kujifunza na kufundisha wengine juu ya asili ya Kanisa. Kadiri wanafunzi wako watakavyoelewa zaidi juu ya asili ya Kanisa, ndivyo itakavyokuwa bora kwao kueleza na kusaidia kufafanua kwa wanafunzi wao kuhusiana na kazi na huduma ya Kanisa. Moja inahusiana moja kwa moja na nyingine. Kadiri wanavyoweza kuliona Kanisa jinsi Mungu anavyoliona, ndivyo watakavyokuwa na uwezo wa kubadilika zaidi katika namna yao ya kulitazama Kanisa katika huduma mpya na bora ndani ya jamii yao wenyewe, na taifa na dunia kwa ujumla. Katika kuwasaidia wanafunzi wako kutafakari hali zao wenyewe, unaweza kubuni baadhi ya maswali au kutumia yale yaliyotolewa hapa chini kama namna ya kuchochea shauku zao. Kilicho muhimu hapa sio maswali yaliyoandikwa hapa chini, bali ni kwamba, katika mazungumzo na wanafunzi wako, uweze kutatua kada ya masuala, wasiwasi, maswali, na mawazo ambayo yanatokana moja kwa moja na mazingira yao ya maisha, huduma na uzoefu wao. Usisite kutumia muda mwingi kwa swali fulani lililotokana na video, au hoja fulani maalum ambayo ni ya msingi hasa katika muktadha wa huduma zao hivi sasa. Lengo la sehemu hii ni ili upate kuwawezesha kufikiri kwa kina na kitheolojia kuhusiana na maisha yao wenyewe na mazingira yao ya huduma. Kwa mara nyingine tena, maswali yaliyo hapa chini yametolewa kama miongozo na vitangulizi, na hayapaswi kuonekana kama ya lazima. Uwe huru kuchagua yale unayoona yanafaha kutumika, au kutengeneza ya kwako mwenyewe.

 15 Ukurasa 36 Muhtasari wa Dhana Muhimu

 16 Ukurasa 37 Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Wanafunzi

Made with FlippingBook - Share PDF online