Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
2 2 6 /
THEOLOJIA YA KANISA
Sehemu hii ya somo inadai kwamba wewe kama mkufunzi uzingatie moja kwa moja umuhimu wa dhana hizi kwa uzoefu na changamoto za wanafunzi kwa ujumla. Kwa maneno mengine, ni jinsi gani masuala ya uchaguzi wa Mungu kwa Kanisa na ufunuo wake kivuli kupitia Israeli, namna ambavyo wokovu kama ushiriki katika Kanisa, yanahusiana hasa na muktadha wao na maswali yao. Bila shaka, inawezekana kutengeneza miunganiko kati ya mawazo haya na uzoefu wao, na kazi yako ni kuchunguza njia ambazo miunganiko hii inaweza kutambuliwa na kufuatiliwa katika mazungumzo ya pamoja kwa faida ya uelewa na kujengana. Vielelezo katika sehemu hii vinahusiana moja kwa moja na baadhi ya dhana zilizotolewa katika sehemu ya ufundishaji ya somo hili. Masomo haya yanasisitiza haja ya kuwa na utambuzi kuhusu asili ya watu wa kweli wa Mungu, hasa ni nani anayepaswa kujumuishwa au kuachwa, na jinsi tunavyopaswa kujua sifa zinazowatambulisha watu wa Mungu tukizingatia yale ambayo yamezungumziwa katika somo hili. Katika mjadala wako na wanafunzi sisitiza hitaji lao la kuwa na ufahamu wa kina wa namna Mungu anavyojumuisha watu katika jamii ya “watu wake” linapokuja kwa wale wanaomkubali na kumwamini Kristo kwa ajili ya wokovu wao binafsi. Ni muhimu kukumbuka kwamba mwelekeo wa wanaume na wanawake wa imani, hata wale walio waadilifu zaidi (k.m., Petro), ni kuwekea kikomo fadhili na upendo wa Mungu kwa wale walio kama sisi, wanaoamini katika kila jambo tunalofanya, wanaotenda na kuabudu kama tupendavyo, na wanaokazia mawazo ya mafundisho na masuala ambayo tumeona kuwa ya kusadikisha. Hata hivyo, Mungu amewachagua Wayahudi na Wasio Wayahudi kuwa sehemu ya jamii yake mpya ya wanadamu, na akathibitisha kwamba wokovu unahusishwa moja kwa moja na watu wake wapya, hata wale ambao tunaweza kupata ugumu kuhusiana nao au kuwafurahia. Chaguo si letu bali ni la Bwana, na tumeitwa kuwapenda na kuwakumbatia wale wote wanaomkaribisha Kristo maishani mwao kama Bwana wa wote. Kutokana na masomo haya, ibua mawazo haya na mengine yanayohusiana nayo ambayo yanaweza kuwasaidia wanafunzi wako kutambua ushabiki na ukosoaji wao dhidi ya wale ambao wanaweza kuwa tofauti nao.
17 Ukurasa 39 Mifano Halisi
Made with FlippingBook - Share PDF online