Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 2 2 7

THEOLOJIA YA KANISA

Uhusianishaji wa somo na huduma unapaswa kuwa uhusianishaji safi zaidi, wa moja kwa moja, na wa kibinafsi zaidi ambao kila mwanafunzi anaweza kufanya ili kuhusisha dhana hizi na uzoefu fulani mahususi alionao, iwe katika maisha yake binafsi au maisha ya wale ambao anatumikia ndani ya kanisa na kupitia kanisa lake. Tuna mwelekeo wa kutumia mambo katika maisha yetu pale tu ambapo tunaweza kugundua uhusiano na miunganiko iliyopo kati ya umuhimu na uhalali wa dhana au kweli fulani na shauku au hitaji fulani kubwa la maisha yetu. Tafuta kuwasaidia wanafunzi kugundua hitaji au suala muhimu zaidi walilo nalo, na kuwawezesha kuona jinsi kweli hizi zinavyoweza kujibu baadhi ya maswali yao, kutatua masuala ya maisha na huduma zao, kuangazia mambo fulani katika uzoefu wao wa maisha na huduma, au hata kuwapa maarifa kuhusu mielekeo mipya wanayopaswa kuchukua. Ombea wanafunzi wako kwa bidii kwamba Bwana Roho Mtakatifu awafundishe kupitia muda uliosalia utakaokuwa pamoja nao, na muda ambao wanafunzi watakuwa nao pamoja wao kwa wao. Tena, kumbuka kile Yesu alichofundisha kuhusu Roho Mtakatifu na suala la “kweli”: Yohana 16:13 – Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yesu atataka kufanya miunganisho kwa kila mwanafunzi, kwa hivyo kuwa mwangalifu kuwaelekeza kwenye sehemu inayofaa ya mawasiliano ambayo inaweza kuwa muhimu zaidi kwao kwa wakati huu. Maandiko yanathibitisha wazi wazi kwamba kuna uhusiano wa karibu sana kati ya huduma ya Neno na maombi. Hili liko dhahiri hasa katika huduma ya mitume wanapotatua mgogoro juu ya mgao wa chakula na mahitaji kwa wajane wa Kiyunani (rej. Mdo. 6:1-). Walipojaribiwa kuingia katika mzozo wa kanisa juu ya ugawaji sahihi wa mahitaji ndani ya kanisa, mitume walihimiza Kanisa kuchagua wawakilishi wenye sifa na ukomavu kiroho ili kutatua mambo hayo, bali wao wangejishughulisha tu na huduma ya neno na maombi (Mdo. 6:4 - na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno). Kwa hakika, maombi yanasisitizwa kwanza katika kifungu hiki, ikidokeza kwamba kuna uhusiano wa karibu kati ya maombi yenye bidii yaliyojaa imani na matumizi yenye matokeo ya

 18 Ukurasa 41 Kuhusianisha Somo na Huduma

 19 Ukurasa 41 Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook - Share PDF online