Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

2 2 8 /

THEOLOJIA YA KANISA

Neno la Mungu. Daima acha muda wa kutosha wa kuomba pamoja na wanafunzi kuhusu kweli ambazo wamezigundua katika Neno. Roho Mtakatifu anaweza kutumia maombi yao ili kuimarisha kweli hizo katika mioyo yao, na kuamsha shauku na mzigo mpya na wa tofauti ndani ya wanafunzi kutokana na kumsikiliza Mungu katika maombi. Kila inapowezekana, jitahidi kupatikana ili kuomba pamoja na wanafunzi kuhusu maeneo mahususi ambayo watagundua kuwa yana umuhimu mkubwa kwao kupitia ufundishaji wako wa somo hili. Hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa kazi za wiki ijayo, hasa ile ya kuandika. Hili si jambo ngumu; lengo ni kwamba wasome maeneo waliyoagizwa vizuri kadiri wawezavyo na kuandika sentensi chache juu ya kile wanachodhani kimemaanishwa. Huu ni ujuzi muhimu wa kiakili kwa wanafunzi wako kujifunza, kwa hivyo hakikisha kwamba unawatia moyo katika mchakato huu. Bila shaka, kwa wale wanafunzi ambao wanaweza kuona hili kuwa gumu, wahakikishie kuhusu dhamira ya zoezi hili, na usisitize kwamba jambo muhimu ni uelewa wao wa kile walichosoma, na si weledi wao katika uandishi. Tunataka kuboresha ujuzi wao, lakini si kwa namna inayoharibu juhudi za kuwatia moyo na kuwajenga. Pamoja na hayo, hatutaki pia kudunisha uwezo wao kwa namna yoyote. Tafuta namna ya kuweka uwiano mzuri kati ya kuwapa changamoto na kuwatia moyo.

 20 Ukurasa 42 Kazi

Made with FlippingBook - Share PDF online