Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
2 3 0 /
THEOLOJIA YA KANISA
pamoja na kutafakari juu ya masuala ya kitheolojia yanayohusika. Tafadhali soma kwa umakini malengo yafuatayo. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo unavyoongeza uwezekano wao wa kuelewa na kufahamu kweli muhimu ambazo ndio msingi wa somo hili.
Ibada hii inazingatia nia na msukumo wa sifa na ibada zote zinazomwadhimisha Mungu: utukufu usio na kifani wa nafsi ya Mungu, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Mara nyingi tunaweza kufikiri kwamba ibada inahusisha aina fulani ya matendo ya kiibada, taratibu za sherehe za kidini, au utaratibu wa kiliturujia. Ibada ya Mungu haina mizizi katika jiografia au mafundisho ya kidini, bali, kama Yesu asemavyo, katika “roho na kweli” (Yn. 4:24). Baba hawezi kukaribiwa isipokuwa kwa njia ya Yesu Kristo (Yn. 14:6), ambaye dhabihu yake ya upatanisho imetuleta karibu na Mungu kwa imani (Ebr. 10:22-24). Kwa sababu Mungu ametujalia sisi kuingia katika uwepo wake, yaani, Patakatifu pa patakatifu kwa damu ya Yesu, na kwa sababu utukufu wa Mungu haulinganishwi na haubadiliki, tunaendelea kuwa na sababu iliyo sahihi ya kumpa Mungu utukufu na heshima. Hatuhitaji kamwe kungoja hali ziwe nzuri na zenye kuvutia ajabu ili kumsifu Mungu; hata katikati ya janga la kutisha, hasara kubwa zaidi, uadui, na hitaji kuu zaidi, tunapaswa kutoa sifa na utukufu kwa Mungu. Licha ya yote tunayokabiliana nayo na yote tuanayoyajua, yeye ni Bwana wa yote, mkamilifu, mtukufu, mkuu, aliyejaa adhama na maajabu, ambaye hatatuacha wala kututupa kamwe. Bila kujali jinsi mambo yanavyoonekana, Mungu yuko na anabaki milele upande wetu na kwa ajili yetu. Kujifunza kutoa “dhabihu” ya sifa, tukibadilisha maana ya neno hili kwa muda, ni ujuzi mkuu ambao mwanafunzi wa Yesu anayekua anapaswa kuwa nao. Mara nyingi tutakabiliana na hali ambapo, kwa kuiangalia juu juu hali hiyo, hatuoni sababu hata moja ya kumsifu Mungu. Kila kitu kimekaa vibaya na giza; Mungu anaonekana kama hayupo, ama hajui, au hajali, au hawezi kusaidia. Katikati ya aina hii ya taabu, tushike vinubi vyetu na kumpa utukufu Yeye atupaye uhai na kutegemeza siku zetu. Anastahili kwa kuwa anastahili, kwa maana Jina lake ni “Niko Ambaye Niko.” Wape changamoto wanafunzi kuhusu wito wao wa kweli, sifa isiyoharibika na isiyo na kikomo kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya asili yake na kile ambacho amefanya katika Yesu Kristo.
2 Ukurasa 45 Ibada
Made with FlippingBook - Share PDF online