Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 2 3 1
THEOLOJIA YA KANISA
Mtunga Zaburi anathibitisha uwezo wa Neno la Mungu kufanya njia yetu kuwa safi (Zab. 119:9), kulinda dhidi ya nguvu za dhambi (Zab. 119:11), na kumpa uzima yeye anayelipokea (Zab. 119:93). Usigeuze muda wa kukariri Maandiko kuwa zoezi la kazi la darasani lililojawa na taratibu na marudio ya kuchosha. Tumia wakati huu kuwapa changamoto na kuwafundisha wanafunzi juu ya manufaa ya Neno lililokaririwa. Kariri Maandiko pamoja na wanafunzi, na upitie upya pamoja nao pale unapoweza. Jadili maana ya Maandiko, na jinsi yanavyohusiana kimaudhui na yale yaliyoshughulikiwa katika somo juma lililopita. Sehemu hii ya somo inaweza kuwa muhimu zaidi, kwa hivyo ichukue kwa umuhimu na heshima inayohitajika. Ni rahisi sana kulemewa na kulichukulia Neno lililokaririwa kama jambo rahisi la kutimiza kwa hitaji la somo. Kama mkufunzi, jaribu kulinda kipengele hiki dhidi ya kosa hili. Acha wanafunzi wajadili kwa ufupi katika vikundi jinsi utambuzi huu ulivyotokea. (Hakuna wakati kwa kila mtu kutoa ushuhuda wake wote kwa hivyo hakikisha wanafunzi wanazingatia jambo maalum la wakati walipoelewa kuwa hawawezi kupata wokovu kwa jitihada zao). Warudishe wanafunzi pamoja na zungumza maneno haya: “Kanisa lipo kwa sababu ya neema ya Mungu pekee. Somo la leo linatusaidia kuelewa ibada kama mwitikio wa Kanisa kwa neema.” Sehemu hizi mbili za mwisho za Kujenga Daraja zinashughulikia mada inayofanana, yaani, tabia na ubora wa ibada yetu, na kile ambacho Mungu anataka au anakihitaji. Kilicho muhimu katika kuzingatia ibada hapa ni kanuni za kitamaduni na kijamii zinazohusiana na mazoea na matukio yanayochukuliwa kuwa ibada. Kwa maneno mengine, makanisa kwa kiasi kikubwa hayatambui kwamba ibada zao huwa zimeundwa kitamaduni na kihistoria, na kwamba ibada ya Mungu, kama madhihirisho ya ukweli na moyo, lazima iwe na sifa ya kuwa ya kina, ya kibinafsi, na ya moja kwa moja. Kamwe haitakuwa ibada kwa kupenda tu yale ambayo wengine wamefanya, tukitazamia hisia na shauku ambazo walikuwa nazo zitokezwe tena ndani yetu kwa kufanya tu matendo yao, kuimba nyimbo zao, au kuyaishi matendo yao. Ibada, kama madhihirisho ya Roho, kila mara itavikwa mavazi ya utamaduni lakini pia itatolewa kila wakati kwa Mungu aliye juu ya tamaduni zote, Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu. Kuwepo na kubadilika kwa mitindo na mbinu za kuabudu kunahusiana moja kwa moja na kuona kwamba
3 Ukurasa 47 Mapitio ya Kukariri Maandiko
4 Ukurasa 47 Kujenga Daraja – Sehemu ya 1
5 Ukurasa 47 Kujenga Daraja – Sehemu ya 2 na ya 3
Made with FlippingBook - Share PDF online