Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

124

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

Mapokeo, mwendelezo

Aimee Semple McPherson wa Kanisa la Foursquare), na vile vile walio wachache (k.m., Richard Allen wa Kanisa la Maaskofu wa Kiafrika wa Methodisti au Charles H. Mason wa Kanisa la Mungu la katika Kristo, ambaye pia alisaidia kuibua Assemblies of God), wote hawa walijaribu kuelezea Mapokeo ya Kimamlaka na Mapokeo Makuu kwa namna maalum. Kuibuka kwa harakati muhimu, zenye nguvu ya imani kwa nyakati tofauti na kati ya watu mbalimbali kunaonyesha utendaji mpya wa Roho Mtakatifu katika historia. Kwa hiyo, ndani ya Ukatoliki, jumuiya mpya zimezuka kama vile Wabenediktini, Wafransisko, na Wadominika; na nje ya Ukatoliki, madhehebu mapya yameibuka (Walutheri, Wapresbiteri, Wamethodisti, Kanisa la Mungu katika Kristo, n.k.). Kila moja ya mapokeo haya maalum ina «waanzilishi,» viongozi wakuu ambao nguvu na maono yao yalisaidia kuanzisha madhihirisho ya kipekee ya imani ya Kikristo na desturi za Kikristo. Bila shaka, ili kuwa halali, harakati hizi lazima zifuate na zieleze kwa uaminifu Mapokeo ya ki Mamlaka na Mapokeo Makuu. Washirika wa mapokeo haya maalum wanashikilia desturi zao wenyewe na mifumo ya hali ya kiroho, lakini sifa hizi mahususi si za lazima kwa Kanisa kwa ujumla. Zinawakilisha udhihirisho wa uelewa wa jumuiya husika na uaminifu wake kwa Mapokeo y Kimamlaka na yale Makuu. Mapokeo husika hutafuta kuelezea na kuuishi uaminifu kwa Mapokeo ya ki Mamlaka na Makuu kupitia ibada zao, mafundisho, na huduma. Wanatafuta kuifanya Injili iwe wazi ndani ya tamaduni mpya au tamaduni ndogo, wakizungumza na kuweka kielelezo cha tumaini la Kristo katika hali mpya zinazoundwa na maswali yake zenyewe yanayoulizwa kulingana na hali zake za kipekee. Kwa hivyo, harakati hizi, zinatafuta kupenyeza kwenye muktadha Mapokeo ya ki Mamlaka kwa njia ambayo kwa uaminifu na kwa ufanisi itayapeleka makundi mapya ya watu kwenye imani katika Yesu Kristo, na kuwaingiza wale wanaoamini katika jumuiya ya imani inayotii mafundisho yake na kutoa ushuhuda wake kwa wengine.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software