Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

Viambatisho

125

Mapokeo, mwendelezo

Kiambatisho B

Kufafanua “Mapokeo Makuu”

Mapokeo Makuu (wakati mwingine huitwa “mapokeo ya Ukristo wa kale”) yanafafanuliwa na Robert E. Webber kama ifuatavyo:

[Ni] muhtasari mpana wa imani na desturi ya Kikristo iliyositawishwa kutoka katika Maandiko kati ya wakati wa Kristo na katikati ya karne ya tano.

~ Webber. The Majestic Tapestry . Nashville: Thomas Nelson Publishers, 1986. p. 10.

Mapokeo haya yanathibitishwa sana na wanatheolojia wa Kiprotestanti wa zamani na wa kisasa.

Kwa hiyo mabaraza yale ya kale ya Nikea, Konstantinopoli, lile la kwanza la Efeso, Kalsedonia, na mengine kama hayo, ambayo yaliitishwa kwa ajili ya kukanusha makosa, tunayakubali kwa hiari, na heshima kama matakatifu, maadamu yanahusiana na mafundisho ya imani, kwa kuwa hayana chochote ila tafsiri safi na ya kweli ya Maandiko, ambayo Mababa watakatifu wa kiroho walikuwa wameipokea kwa uangalifu na kuipitisha.

~ John Calvin. Institutes . IV, ix. 8.

. . . mengi ya yale yenye thamani ya kudumu katika uchambuzi wa kisasa wa Biblia yaligunduliwa katika karne ya tano.

~ Thomas C. Oden. The Word of Life . San Francisco: HarperSanFrancisco, 1989. p. xi

Mabaraza manne ya kwanza ndiyo yaliyo muhimu zaidi, kwani yalileta utatuzi kwa imani ya kiorthodox juu ya Utatu na Umwilisho.

~ Philip Schaff. The Creeds of Christendom . Vol. 1. Grand Rapids: Baker Book House, 1996. p. 44.

Kwa hiyo, rejea yetu kwa Mabaraza ya Kiekumene na Imani, inalenga kwa Mabaraza hayo ambayo yanashikilia mapatano yaliyoenea katika Kanisa kati ya Wakatoliki, Waorthodoksi, na Waprotestanti. Ingawa Wakatoliki na Waorthodoksi wanashiriki makubaliano ya pamoja kwenye mabaraza saba ya kwanza, Waprotestanti wanakubali na kutumia hasa manne ya kwanza. Kwa hiyo, mabaraza yale ambayo kanisa zima linaendelea kuyashiriki yanakamilishwa na Baraza la Kalkedon mnamo 451.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software