Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
138
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
Kiambatisho cha 24 Kukabidhi Amana ya Kitume Kupitisha Hadithi kupitia Ufuasi na Mapokeo Mch. Dkt. Don L. Davis
Linda Amana Nzuri
Linda Hadithi Uliyokabidhiwa 1 Tim. 6:20 - Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo 2 The. 3:6 - Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu
2 Tim. 1:13-14 - Shika kielelezo cha maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo ulio katika Kristo Yesu. 14 Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu. 2 Tim. 3:10-11 - Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo
Paulo
wangu, na makusudi yangu, na imani, na uvumilivu, 11 na upendo, na saburi; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika
Timotheo na Mashahidi Wengi
Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote.
Vivyo hivyo uwakabidhi watu waaminifu
Atakaeweza Kuwafundisha Wengine pia
2 Tim 2:2 - a mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.
Ufunguo wa kuongeza wanafunzi ni kuwaandaa wengine kwa hadithi, kweli, desturi, na mapokeo yale yale ambayo mitume walikabidhi kwa wanafunzi wao waaminifu, ambao kwa kumtii Kristo waliyapitisha katika vizazi vyote, hata kwetu sisi. Ni nini msingi wa mapokeo haya? Ni hadithi ya matendo ya Mungu ya kuokoa katika Kristo - kuja kwake, kufanyika mwili, mateso, kusulubishwa, kuzikwa, kufufuka, kupaa, kuwepo mbinguni, na Ujio wa Pili. Walikuwa mashuhuda wa macho wa Ukuu wake, na waliamuru kanisa lake lienende inavyostahili wito wao, likishuhudia kwa maneno na matendo juu ya tumaini la kurudi kwake. Kutengeneza wafuasi ni kuwakita watu katika Hadithi hii ya Mungu katika Kristo katikati ya kusanyiko la Kikristo, inayoonyeshwa katika hali ya kiroho ya pamoja na kupitia utambulisho mmoja - katika ibada, imani, huduma, na ushuhuda.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software