Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
140
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
Krama za Kiroho Zilivyotajwa Hasa katika Agano Jipya, mwendelezo
Ujasiri uliovuviwa kiroho, hekima, ari, na bidii inayowatia moyo na kuwaongoza wengine ili waweze kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Kanisa. Huruma ya moyo ambayo humwezesha mtu kuwahurumia na kuwahudumia kwa moyo mkunjufu wale walio wagonjwa, wanaoumia, au waliokata tamaa.
Uongozi
Rum. 12:8
Rehema
Rum. 12:8
Kuhudumia (au Utumishi, au Kusaidia, au Ukarimu)
Uwezo wa kufanya kwa furaha kazi yoyote ambayo inawanufaisha wengine na kukidhi mahitaji yao ya kimwili (hasa kwa niaba ya maskini au wanaoteseka)
Rum. 12:7; 1 Pet. 4:9
Uwezo wa kukabiliana na uovu na kutenda mema katika namna zinazofanya kuonekana kwa nguvu na uwepo wa ajabu wa Mungu.
1 Kor. 12:10; 12:28
Miujiza
Shauku na uwezo wa kuongoza, kulinda, na kuandaa washiriki wa kusanyiko kwa ajili ya huduma
Uchungaji
Efe. 4:11
Uwezo wa kupokea na kutangaza kwa uwazi ujumbe uliofunuliwa kutoka kwa Mungu ambao unalitayarisha Kanisa kwa utii kwake na kwa Maandiko.
1 Kor. 12:28; Rom. 12:6
Unabii
1 Kor. 12:28; Rum. 12:7; Efe. 4:11
Uwezo wa kueleza maana ya Neno la Mungu na matumizi yake kupitia mafundisho makini
Ualimu
Kunena kwa Lugha
1 Kor. 12:10; 12:28
Matamshi ya kusisimua ambayo kwayo mtu huzungumza na Mungu (au wengine) chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu
Ufahamu uliofunuliwa na Roho ambao huruhusu mtu kunena maagizo ya kimungu kwa ajili ya kutatua matatizo; na/au Ufahamu uliofunuliwa na Roho unaomruhusu mtu kueleza siri kuu za imani ya Kikristo
Hekima
1 Kor. 12:8
Made with FlippingBook Digital Publishing Software