Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Viambatisho
141
Kiambatisho cha 26 Tamko Letu la Utegemezi: Uhuru Katika Kristo Mch. Dkt. Don L. Davis, Januari 11, 2003
Ni muhimu kufundisha maadili katika mwangaza wa uhuru (yaani., Gal. 5:1, “Katika ungwana huo Kristo alituandika huru”), na daima katika muktadha wa kutumia uhuru wako katika mfumo wa kumletea Mungu utukufu na kueneza Ufalme wa Kristo. Nasisitiza kanuni ya “6-8-10” za 1 Wakorintho, na kuzitumia katika mambo yote ya kimaadili. 1. 1 Kor. 6:9-11, Ukristo ni kwa habari ya badiliko katika Kristo; hakuna kiasi cha visingizio kitakachomwingiza mtu katika Ufalme.
2. 1 Kor. 6:12a, Tuko huru katika Kristo, lakini si kila kitu anachofanya mtu ni kinajenga au kusaidia.
3. 1 Kor. 6:12b, Tuko huru katika Kristo, lakini chochote chenye uwezo wa kututawala ni kinyume na Kristo na Ufalme wake.
4. 1 Kor. 8:7-13, Tuko huru katika Kristo, lakini hatupaswi kamwe kujivunia uhuru wetu, hasa mbele ya Wakristo ambao dhamiri zao zingeharibiwa na ambao wangejikwaa ikiwa wangetuona tukifanya jambo kwao lingekuwa la kukwaza. 5. 1 Kor. 10:23, Tuko huru katika Kristo; vitu vyote ni halali kwetu, lakini si kila kitu kinafaa au kinauwezo] wa kujenga nafsi. 6. 1 Kor. 10:24, Tuko huru katika Kristo, na tunapaswa kutumia uhuru wetu kuwapenda kaka na dada zetu katika Kristo, na kuwalea kwa ajili ya ustawi wa wengine (rej. Gal. 5:13). 7. 1 Cor. 10.31, Tuko huru katika Kristo, na tumepewa uhuru huo ili tuweze kumtukuza Mungu katika yote tunayofanya, iwe katika kula au kunywa, au chochote kingine.
8. 1 Kor. 10:32-33, Tuko huru katika Kristo, na tunapaswa kutumia uhuru wetu ili kufanya kile tuwezacho ili
kutowakosea watu katika ulimwengu au Kanisa, lakini tufanye kile tunachofanya ili kuwashawishi kumjua na kumpenda Kristo, yaani, wapate kuokolewa.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software