Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
142
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
Tamko Letu la Utegemezi: Uhuru Katika Kristo, mwendelezo
Pamoja na kanuni hizi, naamini tunapaswa pia kusisitiza kanuni zifuatazo:
• 1 Pet. 2:16 – Tunapaswa kuuishi uhuru wetu katika Kristo kama watumishi wa Mungu, lakini kamwe tusitafute kutumia uhuru wetu kama kifuniko cha uovu. • Yn. 8:31-32 – Tunajionyesha kuwa wanafunzi wa Kristo tunapokaa na kuendelea katika neno lake, na kwa kufanya hivyo tunapata kujua kweli, na kweli hutuweka huru ndani yake. • Gal. 5:13 – Sisi, kama ndugu, tuiitwa tupate uhuru; lakini uhuru wetu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali kutumikiana kwa upendo Katika akili yangu, msisitizo huu wa uhuru, unayaweka mambo yote tunayosema kwa watu wazima au vijana katika muktadha. Mara nyingi, jinsi Wakristo wengi wapya wanavyofunzwa ni kupitia kuorodhesha makosa mbalimbali, na wakati fulani hii inaweza kuwapa hisia kwamba Ukristo ni dini ambayo si ya kimatendo (dini ya kutofanya mambo tu), na/au imani inayoshughulika sana na kutotenda dhambi. Kimsingi, mkazo wa kiadili katika Ukristo ni uhuru, uhuru uliopatikana kwa gharama ya juu, uhuru wa kumpenda Mungu na kueneza Ufalme, uhuru wa kuishi maisha ya unyenyekevu mbele za Bwana. Wajibu wa kimaadili wa Wakristo wa mijini ni kuuishi uhuru katika Yesu Kristo, kuishi huru kwa utukufu wa Mungu, na kutotumia uhuru wao kutoka kwa sheria kama kibali cha dhambi. Kwa hiyo, kiini cha mafundisho haya, ni kuzingatia uhuru tuliopata kupitia kifo na ufufuo wa Kristo, na muungano wetu naye. Sasa tumewekwa huru kutoka kwa sheria, kanuni ya dhambi na mauti, hukumu na hatia ya dhambi zetu wenyewe, na mashtaka ya sheria juu yetu. Sasa tunamtumikia Mungu kama tendo la shukrani, na msukumo mkuu wa maadili ni kuishi kwa uhuru katika Kristo. Hata hivyo, hatutumii uhuru wetu kuwa watu wenye hekima au watu wenye akili, bali kumtukuza Mungu na kuwapenda wengine. Huu ndio muktadha ambao tunashughulikia maswala ambayo yamekuwa mchongoma kama ushoga, utoaji mimba, na maovu mengine ya kijamii. Wale wanaojihusisha na vitendo hivyo hujifanya kuwa huru, lakini, kwa kukosa ujuzi wa Mungu katika Kristo, wanafuata tu mielekeo yao ya ndani, ambayo si ufahamu wa mapenzi ya Mungu ya kiadili au upendo wake.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software