Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

156

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

Kiambatisho cha 37 Orodha ya Mambo ya Kuzingatia kwa ajili ya Utumishi wa Kiroho Mch. Dkt. Don L. Davis

1. Wokovu : Je, mtu huyu ameamini Injili, amemkiri Yesu kama Bwana na Mwokozi, amebatizwa, na kujiunga rasmi na kanisa letu kama mshirika? 2. Uadilifu Binafsi : Je, anatembea na Mungu, kukua katika maisha yake binafsi, na kuonyesha upendo na uaminifu katika familia, kazi, na jamii?? 3. Kuandaliwa Katika Neno : Je, mtu huyu ameandaliwa vipi katika Neno la Mungu ili kushiriki na kufundisha na wengine?? 4. Msaada kwa kanisa letu : Je, anasaidia kanisa kupitia uwepo wake, maombi kwa ajili ya viongozi na washiriki, na kutoa msaada wa kifedha kwa kanisa?

5. Unyenyekevu kwa mamlaka : Je, mtu huyu ananyenyekea kwa furaha kwa mamlaka ya kiroho?

6. Utambulisho wa karama za kiroho : Je, ni karama, vipaji, uwezo, au rasilimali gani mtu huyu anazo kwa ajili ya huduma, na ana mzigo gani hasa wa huduma kwa sasa.?

7. Upatikanaji wa Sasa : Je, yuko tayari kupewa kazi au mradi ambapo tunaweza kutumia huduma yake kujenga mwili?

8. Sifa miongoni mwa viongozi : Je, viongozi wengine wanahisije kuhusu utayari wa mtu huyu kwa nafasi mpya ya uongozi?

9. Rasilimali zinazohitajika kukamilisha : Iwapo atateuliwa kwa jukumu hili, ni mafunzo gani, pesa, rasilimali na/au mchango gani atahitaji ili kukamilisha kazi hiyo?

10. Agizo rasmi : Ni lini na jinsi gani tutawajulisha wengine kwamba tumemteua mtu huyu kwa kazi au mradi wao?

11. Muda na kutoa taarifa : Pia, tukimweka wakfu mtu huyu kwa jukumu/kazi hii, ataweza kuanza lini, na anapaswa kuhudumu kwa muda gani kabla hatujamtathmini.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software