Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
164
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
Wajibu wa Wanawake katika Huduma, mwendelezo
walitekeleza katika upanuzi wa Ufalme na maendeleo ya kanisa katika karne ya kwanza. Wanawake walihusika katika huduma za unabii na maombi (1Kor. 11:5), mafunzo ya binafsi (Mdo 18:26), mafundisho (Tito 2:4, 5), kutoa shuhuda (Yoh. 4:28, 29), ukarimu (Mdo. 12:12) na walitumika kama watenda kazi wenza wa mitume katika kuhubiri Injili (Flp. 4:2-3). Paulo hakuwaweka wanawake nafasi ya chini au hadhi iliyofichwa bali alitumika bega kwa bega na wanawake kwa ajili ya Kristo “Namsihi Euodia, namsihi na Sintike, wawe na nia moja katika Bwana. 4.3 Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.” (Flp. 4.2-3). Zaidi ya hayo, ni lazima tuwe waangalifu katika kuwanyenyekeza wanawake (yaani, asili yao kama wanawake) dhidi ya nafasi yao ya unyenyekevu katika uhusiano wa ndoa. Ijapokuwa maelezo ya wazi ya jukumu la wanawake kama warithi pamoja wa neema ya uzima katika uhusiano wa ndoa (1 Pet. 3.7), ni wazi vile vile kwamba Ufalme wa Mungu umeibua badiliko kubwa la jinsi wanawake wapasavyo kutazamwa, kueleweka, na kukumbatiwa katika jumuiya ya Ufalme. Ni wazi kwamba katika Kristo sasa hakuna tofauti kati ya tajiri na maskini, Myahudi na Myunani, mgeni, Msikithi, mtumwa na mtu huru, na vilevile mwanamume na mwanamke (taz. Gal. 3:28; Kol. 3.11). Wanawake waliruhusiwa kuwa wanafunzi wa Rabi (jambo ambalo lilikuwa geni na lilikataliwa wakati wa Yesu), na walitekeleza majukumu mashuhuri katika kanisa la Agano Jipya, ikijumuisha kuwa watenda kazi wenzi bega kwa bega na mitume katika huduma (k.m., tazama Euodia na Sintike katika Flp. 4.1 na kuendelea), pamoja na kukaribisha kanisa katika nyumba zao (taz.1-2, 6 Fibi; Filem 1). Kuhusiana na suala la mamlaka ya kichungaji, nina hakika kwamba uelewa wa Paulo wa jukumu la uandaaji (ambalo hufanywa na mchungaji-mwalimu, cf. Efe. 4.9-15) si la kjinsia. Kwa maneno mengine, maandiko yanayoweza kuamua na ya mwisho kwa ajili yangu juu ya utendaji wa karama na hadhi na kazi ya ofisi ni maandiko ya Agano Jipya ambayo yanahusu karama (1 Kor. 12:1-27; Rum. 12.4-8; 1 Pet. 4:10-11, na Efe. 4:9-15). Hakuna dalili katika yoyote ya maandiko haya kwamba karama ni mahususi kwa jinsia. Kwa maneno mengine, ili hoja ishikilie kwa uhakika kwamba wanawake hawakupaswa kamwe kuwa katika majukumu ya uchungaji na uandaaji wa waamini wengine, hoja rahisi na yenye ufanisi zaidi ingekuwa kuonyesha kwamba Roho hawezi hata kufikiria kumpa mwanamke karama ambayo haikuwa inaendana na uelekeo wa wito aliokuwa nao. Wanawake
Made with FlippingBook Digital Publishing Software