Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Kipinidi cha 1 : Utangulizi
17
, kaleo¯ Limetokana na mzizi kal -, ambapo kwenye King. ni “ita” na “kelele” (ona B na C, hapa chini), linatumika (a) kwa mtu binafsi, “kumwita mtu yeyote, kualika, kumwagiza kazi,” k.m., Mt. 20:8; Mt. 25:14; linatumika hasa kwa wito wa Kimungu wa kushiriki baraka za ukombozi, k.m., Rum. 8:30; 1 Kor. 1:9; 1 Thes. 2:12; Ebr. 9:15; rej. B na C, hapa chini; (b) linatumika katika utaratibu wa kutoa majina au wito, kazi au nafasi, «kuita kwa jina, kukipa kitu jina»; katika Kauli ya Kutendwa, «kuitwa kwa jina, kuchukua jina.» Kwa hivyo linatoa maana ya ama wito au hatima; muktadha huamua ni kipi, k.m., Rum. 9:25-26; “jina la ukoo,” katika Matendo 15:37, AV, si sahihi (RV, “iliitwa”).
~ Vine’s Complete Expository Dictionary, New Testament utafutaji-neno, toleo tepe katika programu ya kompyuta
F. Kanuni ya Utoshelevu ya wito wa Mungu
1. Kanuni hii inasema: Mungu kamwe haiti mtu au kikundi cha watu kuwa au kufanya chochote bila
kuwapa vipawa, nyenzo, mahitaji, na fursa ya kutimiza wito huo. Flp. 2:12-13 – Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. 13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.
2. Kanuni hii ilitumika kwa viongozi wa watu wa Mungu: Musa na Yoshua na viongozi wa Agano Jipya.
3. Kanuni hii ilitumika kwa watu wa Mungu: taifa la Israeli na Kanisa.
4. Kila mtu katika Kanisa la Mungu (washirika na viongozi) ameitwa pamoja na wengine ili kuwakilisha sifa, maslahi, na kusudi la Mungu katika maisha yake.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software