Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
52
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
D. Ufahamu wa pekee kwa viongozi wa kiroho: Je, mwito wa uhuru unamwathiri na kumwezesha vipi kiongozi aliyeitwa kuwajenga na kuwatayarisha watu wa Mungu?
1. Kwa wale walioitwa kimaalum, uhuru katika Kristo lazima ufafanuliwe kama suala la kujidhabihu na kupatikana bila masharti kwa huduma ya Kristo kwa ajili ya Injili.
a. Ni lazima wauthamini uhuru tuliopata kwa Yesu Kristo, 1 Tim. 1:12-16 – Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake; 13 ingawa hapo kwanza nalikuwa mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri, lakini nalipata rehema kwa kuwa nalitenda hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani. 14 Na neema ya Bwana wetu ilizidi sana, pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu. 15 Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi. 16 Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele.
b. Wanapaswa kudhihirisha maishani mwao na kuwa na uzoefu halisi wa nguvu ya uhuru wa Roho Mtakatifu (2 Kor. 3:17).
2. Kiwango hiki cha uhuru thabiti huwezesha kuwafanya wale ambao wamepokea wito maalum waweze kuwa vitu vyote kwa watu wote (1 Kor. 9:19-23).
3. Uhuru wa kiongozi unakusudiwa kumfanya awe tayari kubadili uelekeo na kupatikana kwa Mungu kwa ajili ya huduma kwa wengine, 1 Kor. 4:9-13 – Maana nadhani ya kuwa Mungu ametutoa sisi mitume mwisho, kama watu waliohukumiwa wauawe; kwa sababu tumekuwa tamasha kwa dunia; kwa malaika na wanadamu. 10 Sisi
Made with FlippingBook Digital Publishing Software