Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

58

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

dada zangu hao waliweza kuamini wito wangu, wakiwa na imani katika Mungu ambaye huwapa wanadamu karama. . . .Wito wa Mungu unahusiana na kuujenga Mwili wake. Sio kusudi kuu la Mungu kujitukuza kupitia watu binafsi, bali kupitia vikundi vya watu walioitwa kwa jina lake (Efe. 1:18; 3:10). Mungu hakukusudia niwe Mkristo-peke wa kujitenga na kujitegemea. Tangu tufike Mississippi ametupa watu ambao wanaweza kutuunga mkono na kututia moyo na pia kutuwajibisha. Kama mtu binafsi ninaweza kuwa shahidi. Lakini ingawa mimi kama mmishenari ninaweza kuonekana kuwa peke yangu, kuna wengine kila mara wanaosimama karibu nami, wakisali kutoka mbali, au kufanya kazi pamoja nami. Na hiki ndicho kielelezo cha jinsi Mungu anavyotutoa katika hali ya ubinafsi na kutuweka katika mwili (ushirika). Katika mwili, pamoja na karama zote zinazotenda kazi kama mikono na miguu na sehemu nyinginezo, tunafanyika kielelezo halisi cha Yesu Kristo katika mwili, yaani Mwili halisi wa Kristo.

~ John Perkins. A Quiet Revolution . Waco TX: Word Books, 1976. uk. 37.

A. Ufafanuzi wa wito kwa jumuiya katika hadithi ya Kutoka

1. Agizo la Mungu kwa watu wake kuangamiza kabisa mataifa ya Kanaani, Kum. 7:1-2 – Bwana, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang’oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe; 2 wakati Bwana, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao. 2. Shauku ya Mungu kwamba watu wake wawe wa tofauti na wa thamani kwake, Kumb. 7:6 – Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako; Bwana Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.” 3. Agano la Mungu na watu wake: uaminifu wa mtu binafsi kwa agano unaodhihirishwa kupitia maisha ya ushirika ndani ya jumuiya ya Mungu , Kumb. 7:7-10 – Bwana hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana

Made with FlippingBook Digital Publishing Software