Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Kipindi cha 5 : Wito kwa Jumuiya
59
mlikuwa wachache kuliko watu wote; 8 bali kwa sababu Bwana anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu Bwana akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri. 9 Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu; 10 naye huwalipa wamchukiao mbele ya uso wao, kuwaangamiza. Hatakuwa mlegevu kwake yeye amchukiaye, atamlipa mbele ya uso wake.
4. Utiifu kama mshirika mwaminifu wa jumuiya ya agano la Mungu ni ishara ya utiifu wa kweli kwake, Kumb. 7:11 – Basi zishike amri, na sheria, na hukumu ninazokuamuru leo, uzitende.
B. Kanuni kwa watu wa Mungu leo
1. Watu wa Mungu wa agano leo: Kanisa la Yesu Kristo, 2 Kor. 3:4-6 – Na tumaini hilo tunalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo. 5 Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu. 6 Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.
2. Je, watu binafsi wanapataje kuingia katika mwili (ushirika)? Toba na imani (Mdo 17:30-31; Rum. 10:9-10; Yn. 5:24).
3. Je, ni kwa njia gani Mwili unawaingiza wanachama katika ushirika? Ubatizo
a. 1 Kor. 12:12-13 – Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo
Made with FlippingBook Digital Publishing Software