Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Kipindi cha 5 : Wito kwa Jumuiya
61
c. Gal. 6:2
d. Rum. 13:8-10
e. Kol. 3:12-17 – Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, 13 mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. 14 Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. 15 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. 16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. 17 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye. 6. Ninawezaje kuiwakilisha vyema na kwa uaminifu imani na misimamo ya ushirika? Utii kwa mamlaka na kuitumia mamlaka , Ebr. 13:17 – Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.
C. Mifano halisi kuelezea wito kwa jumuiya
1. Wayahudi walioamini huko Yerusalemu siku ya Pentekoste (Mdo 2:42-47).
2. Waamini walioteswa kwa mujibu wa Matendo 4, Mdo. 4:32-35 – Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali
Made with FlippingBook Digital Publishing Software