Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
62
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika. 33 Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. 34 Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa, 35 wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji.
D. Ufahamu wa pekee kwa viongozi wa kiroho: Je, lipi ni jukumu na wajibu wa wale walioitwa kimaalum kuwakilisha jumuiya ya Kikristo?
1. Onyesha kupitia maisha yako ya nidhamu na huduma ufuasi wako kwa Kristo katika mwili wa Kristo.
a. Ni lazima wawe wanafunzi wa Yesu (sio waongofu wa hivi karibuni), 1 Tim. 3:6; 5:22.
b. Ni lazima wawe viungo vya mwili vilivyothibitishwa vyema (taz. 2 Kor. 8:22).
c. Ni lazima wadumishe ushuhuda wenye mvuto katika Kanisa na ulimwengu.
(1) Yak. 3:13 – N’nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.
(2) Kol. 4:5 – Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.
2. Jitiishe chini ya mchakato wa kupokea uthibitisho wa wito wako (kusimikwa au kuwekwa wakfu), Mk. 3:14; Mdo. 14:23.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software