Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
64
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
(6) 1 Tim. 1:11 – Kama vile ilivyonenwa katika Habari Njema ya utukufu wa Mungu ahimidiwaye, niliyowekewa amana. (7) 1 Tim. 6:20 – Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo “elimu” kwa uongo; (8) Mchakato ulioundwa ili kuifunua tabia ya Kristo ndani yako, 1 Tim. 3:1-7; Tito 1:5-9 (yaani, kujitoa kwa Mungu kunakodhihirishwa katika roho ya unyenyekevu, mtindo wa maisha wenye nidhamu, maisha ya familia yenye ucha-Mungu wa kweli, na sifa isiyo na lawama).
e. Utii kwa mchakato ulioundwa ili kudhihirisha kipawa chako na utayari wako wa kufanya kazi kwa ajili ya Kanisa (Flp. 2:19-23; 2 Kor. 8:22).
f. Utii kwa mchakato ulioundwa ili kudhihirisha uelewa wako na utetezi wa fundisho la Mitume (Tito 1:9; 2 Tim. 2:2).
3. Ni lazima utumwe rasmi kufanya kazi kwa sherehe ya utambulisho na kuwekwa wakfu (kuwekewa mikono na askofu na wazee), Mwa. 38:14; Kumb. 34:9; Hes. 27:18 32; Mdo. 6:6; 13:3; 1 Tim. 4:14; 5:22.
a. Kuwekewa mikono (1 Tim. 4:14; 5:22).
b. Kujitoa katika ibada na maombi (Mdo. 6 na 13).
4. Pokea na tumia kwa bidii ipasayo mamlaka na wajibu uliopewa ili kutimiza huduma yako katika mwili wa Kristo.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software