Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

70

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

Flp. 2:4-8 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. 5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; 6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

A. Ufafanuzi wa wito wa huduma katika hadithi ya Kutoka

1. Bwana aliwaita watu wake ili, kwanza kabisa, wawe milki yake ya pekee juu ya watu wote wa dunia.

a. Kum. 4:20 – Bali Bwana amewatwaa ninyi, na kuwatoa katika tanuu ya chuma, katika Misri, mpate kuwa watu wa urithi kwake, kama mlivyo leo hivi.

b. Kumb. 7:6 – Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako; Bwana Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.

c. Kum. 14:2 – Kwa kuwa u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako, na Bwana amekuchagua kuwa watu wake hasa, kuliko mataifa yote yaliyo juu ya uso wa nchi.

d. 1 Fal. 8:53 – Kwa maana uliwatenga na watu wote wa dunia, wawe urithi wako, kama ulivyonena kwa mdomo wa Musa, mtumishi wako, hapo ulipowatoa baba zetu katika Misri, Ee Bwana MUNGU.

e. Zab. 135:4 – Kwa sababu Bwana amejichagulia Yakobo, Na Israeli, wawe watu wake hasa.

2. Wito wa Mungu kwa Israeli baada ya Kutoka ulikuwa ni wito wa wao kujivika na kudhihirisha utakatifu wake katika mahusiano na matendo yao kwa namna ya pekee, Kum. 4:7-8 – Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama Bwana, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo? 8 Tena liko taifa gani kubwa, lililo na amri na hukumu zenye haki kama torati hii yote, ninayoiweka mbele yenu leo.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software