Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Kipindi cha 6 : Wito wa Utumishi
71
3. Wito huu wa ukombozi, utakatifu, uhuru, na jumuiya ya agano ulikusudiwa kuifanya Israeli kuwa nuru kwa mataifa , chombo cha tangazo la Mungu la wokovu kwa mataifa.
a. Isa. 9:1-2 – Lakini yeye aliyekuwa katika dhiki hatakosa changamko. Hapo kwanza aliiingiza nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali katika hali ya kudharauliwa, lakini zamani za mwisho ameifanya kuwa tukufu, karibu na njia ya bahari; ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa. 2 Watu wale waliokwenda katika giza Wameona nuru kuu; Wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, Nuru imewaangaza. b. Isa. 60:1-3 – Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia. 2 Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako. 3 Na mataifa wataijilia nuru yako, Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako. 4. Israeli ilipaswa kutumika kama Mnara wa taa kwa mataifa: kwa kutimiza agano la Mungu, Israeli wangekuwa balozi wa Mungu kwa Mataifa , Isa. 49:6 – naam, asema hivi, “Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.”
B. Kanuni kwa watu wa Mungu leo
1. Ufalme Uliopo/Utakaokuja: watu wa Mungu katika enzi ya Roho
Made with FlippingBook Digital Publishing Software