Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
72
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
a. Enzi ya Roho Mtakatifu imekuja.
(1) Yn. 7:37-39
(2) Lk. 24:44-48
(3) Mdo. 1:8
(4) Mdo. 2:14-21, “hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli. . .”
b. Tit. 2:14 – ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.
c. 1 Pet. 2:9 – Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
2. Karama za Roho: karama na upaji wa Roho, 1 Kor. 12:4 7 – Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. 5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. 6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. 7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.
3. Uongozi wa Roho: fursa na maongozi maalum ya Roho kwa watu waliochaguliwa kwa ajili ya huduma : Paulo
a. Hes. 8:14 – “Ndivyo utakavyowatenga Walawi na kuwatoa katika wana wa Israeli; na Walawi watakuwa wangu.”
Made with FlippingBook Digital Publishing Software