Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Kipindi cha 6 : Wito wa Utumishi
73
b. Mdo. 13:2 – Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, “Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.”
c. Mdo. 22:21 – Naye akaniambia, “Enenda zako; kwa kuwa mimi nitakutuma uende mbali kwa watu wa Mataifa.”
d. Rum. 1:1 – Paulo, mtumwa wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa aihubiri Injili ya Mungu.
e. Rum. 10:15 – Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, “Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!”
f. Gal. 1:15 – Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,
g. 2 Tim. 2:2 – Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine
4. Ubwana wa Kristo uwe hai! Kuishi kama mfuasi wa Kristo katika hali yako ya maisha
a. Kuutambua ubwana wake kama mkuu kuliko mwingine wowote (Rum. 14:7-8).
b. Kuitikia kwa utiifu wa haraka kwa miongozo yake (Yn. 14:13, 21).
Made with FlippingBook Digital Publishing Software